2018-07-04 16:04:00

Viongozi wakuu wa Makanisa watakaoshiriki Siku ya Sala ya Kiekumene


Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki linasema kwamba kutakuwepo na viongozi wakuu pamoja na wawakilishi wa Jumuiya za Kikristo wapatao 18 wanatarajiwa kushiriki katika Siku ya Sala ya Kiekumene kwa ajili ya Mashariki ya Kati. Hawa ni wale wanaotoka kwenye Makanisa ya Kiorthodox chini ya uongozi wa Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiothordox la Costantinopoli, Patriaki Theodoros II wa Kanisa la Alexandria na Afrika katika ujumla wake. Kutakuwepo na mwakilishi wa Askofu mkuu Anthedon; Askofu mkuu Hilarion atakayemwakilisha Patriaki wa Moscow na Urusi nzima. Katika orodha hii, yumo pia Askofu mkuu Vasilios anayemwakilisha Patriaki Chrisostom. Wengine kutoka Makanisa ya Kiorthodox ya Mashariki ni pamoja na Papa Tawadros II; Patriaki Ignatius Aphrem II, Askofu Hovakim anayemwakilisha Patriaki Karekin II pamoja na Patriaki Aram wa I wa Kanisa la Wakatoliki wa Armenia. Kutoka katika Kanisa la Kiorthodox la Siria ni Mar Gewargis II.

Makanisa ya Kikatoliki huko Mashariki yanawakilishwa na  Patriaki Ibrahim wa Kanisa la Kikoptik la Alexandria, Patriaki Ignace Youssif III wa Kanisa la Antiokia ya Siria; Kardinali Bèchara Boutros Rai wa Kanisa la Wamaroniti wa Antiokia na Mashariki yote! Askofu mkuu Jean Clèment Jeanbart wa Kanisa la Kigiriki la Wamelkite; Kardinali Louis Raphael I, Patriaki wa Kanisa Katoliki la Wacaldea wa Babeli. Kardinali Krikor Bedros XX wa Kanisa Katoliki la Waarmenia wa Cilicia pamoja na Askofu mkuu Pierbattista Pizzaballa, Msimamizi mkuu wa Upatriaki wa Yerusalemu. Viongozi wa Jumuiya za Kikristo kutoka Mashariki ya Kati, wanawakilishwa na Askofu Sani Ibrahim Azar wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri nchini Yordan na Nchi Takatifu pamoja na Dr. Souraya Bechealany, Katibu mkuu wa muda wa Baraza la Makanisa ya Mashariki ya Kati.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.