2018-07-02 16:01:00

Askofu Francisco Fortunato de Gouveia ang'atuka kutoka madarakani


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Francisco Fortunato de Gouveia wa Jimbo Katoliki la Oudtshoorn, Afrika ya Kusini. Askofu Francisco Fortunato de Gouveia alizaliwa kunako tarehe 11 Juni 1951 huko Cape Town, Afrika ya Kusini. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akabahatika kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 11 Januari 1976. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Oudtshoorn, Afrika ya Kusini na kuwekwa wakfu kama Askofu hapo tarehe 17 Julai 2010.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.