2018-06-25 16:30:00

Papa: Elimu inazingatia uwajibikaji wa kimaadili kwa binadamu wa leo!


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Mfuko wa Elimu ya Kikristo (Gavissium Educationis), tarehe 25 Juni 2018 mjini Vatican wakiwa katika  fursa ya mkutano wao  mkuu unaongozwa na kauli mbiu “Kuelimisha ni kuunda upya”, mkutano  ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki (Gravissimum Educationis). Amemshukuru Kardinali Vesald i kwa maneno ya hotuba yake na ushiriki wa kila mmoja ambao wanatoa mchango wa utajiri wa uzoefu katika sekta mbaimbali za shughuli mahali wanapotokea.

Baba Mtakatifu Francisko amesema, Mfuko wa Elimu ya Kikristo ulianzishwa mara baada ya kuridhia maombi kutoka Braza la Kipapa la elimu Katoliki mnamo tarehe 28 Oktoba 2015 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 tangu Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican walipochapisha tamko kuhusu umuhimu wa Elimu ya Kikristo (Gravissimum educationis). Hiyo ilikuwa ni kukazia pamoja na mambo mengine, umuhimu wa elimu katika ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Lengo la elimu hiyo katika ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, ni kuwawezesha waamini kufaidika na urithi wa kitamaduni na maisha ya kiroho lakini pia kujenga na kuimarisha mahusiano na mafungamano ya kijamii.

Umuhimu wa maelekezo ya tamko kuhusu umuhimu wa Elimu ya Kikristo uliochapishwa Hati ya Kitume ya Veritatis Gaudium, ili kusaidia mchakato wa waamini kupata elimu, ujuzi na maarifa ya kisayansi ili kuendeleza Elimu Katoliki sehemu mbalimbali za dunia, ni njia ya kubadilisha elimu na dunia inaweza kubadilika na  Kanisa linatambua kwamba, elimu ni sehemu ya haki za msingi za binadamu kwani kila binadamu ana haki ya kupata elimu bora inayoambatana  pia na elimu ya Kikristo. Ni kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ametoa mapendekezo yake. Hawali ya yote ni “kutengeneza  mtandao”. Kutengeneza mtandao maana yake ni kuweka pamoja katiba za shule na Vyuo Vikuu ili kuiviongeza nguvu za kuanzisha elimu na utafiti, kwa kutajirisha sehemu zenye nguvu za kila mmoja  katka ngazi ya kiakili na utamaduni. Kutengeneza mtandao maana yake pia ni kuweka pamoja fahamu, sayansi na maadili katika  kukabiliana na changamoto ngumu za mfano na zinazoendelea katika maadili kama inavyoshuri hati ya  Veritatis Gaudium ( taza n. 4 na kuendelea)

Kutengeneza mtandao maana yake ni kuunda sehemu za makutano na mazungumzo ndani ya taasisi za elimu na kuzihamasisha zaidi hasa  kwa raia wanaokuja kutoka katika tamaduni nyingine, kabila na dini tofauti ili ubinadamu wa kikristo upate kutafakari dunia katika hali ya maisha ya binadamu leo hii.
Kutengeneza mtandao maana yake ni kufanya shule ikiwa ni jumuiya inayo elimisha, na mahali ambapo wakufunzi na hawaunganiki  tu katika mipango ya shule, lakini hata katika mpango mzima wa maisha na uzoefu katika namna ya kuelimishana kwa pamoja kati ya vizazi tofauti. Kwa upande mwingine, changamoto zinazo mgusa mtu wa leo ni za ulimwengu mzima kwa maana ya ukuu wake ulivyo. Elimu haina manaa ya kuunda akili ya mtazamo wa upande  wenye uwezo  wa kukabiliana hali halisi ya mbali tu;  Badala yake Elimu inazingatia kusambaa katika nafasi na uwajibikaji wa kimaadili wa binadamu wa leo na kuendelea kupitia nyakati, na uchaguzi ambao leo hii unatazama kizazi endelevu.
 
Baba Mtakatifu anathibisha kuwa matarajio ya elimu ambayo yanaalika kujibu na ambayo yeye alielekeza katika Waraka wa kitume wa Evengelii Gaudium - Furaha ya Injili  ni ile ya kutoacha kuibiwa matumaini (n.86). Katika ushauri huo aliwatia moyo wanaume na wanawake wa nyakati hizi kukutana kwa uchaya katika maadili ya kijamii na kujikita katika hali halisi katika mwanga ulioangazwa na ahadi ya wokovu wa kikristo. Tunaalikwa kutokupoteza matumaini kwa sababu ni lazima kubaki na  matumaini katika ulimwengu wa leo. Kutoa “utandawazi wa matumaini” na “kusaidia matumaini katika utandawazi” ndiyo shughuli msingi katika utume wa elimu katoliki, kama baba Mtakatifu Francisko  alivyothibitisha katika Waraka wa hivi karibuni kuhusu “Kuelimisha  mshikamano” wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki  taz nn. 18-19). Utandawazi bila matumaini na maono, unajikita kwa masharti ya kiuchumi ambayo daima yako mbali na ustawi wa jamii kwa wote na kusababisha  kwa kasi mivutano ya kijamii, migogoro ya kiuchumi, matumizi mabaya ya utawala. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko anathibitisha kuwa, lazima kutoa uhai katika dunia ya utandawazi kwa njia ya mafundisho ya kiakili na kimaadili ili kutambua namna ya kuchanganua mambo yaliyo mema yatokanayo na utandawazi na kusahihishayale yote yaliyo hasi.

Hiyo inahusiana na upeo muhimu ambo unaweza kufikiwa kwa njia ya maendeleo ya utafiti wa kisayansi, na  ambao umekabidhiwa kwenye vyuo vikuu, vilivyopo katika utume wa Chama cha  Mfuko wa Elimu. Utafiti wa hali  juu na ambao unakabiliana na utajiri wa changamoto. Baadhi ya changanto  hizo zimetajwa katika Wosi wa Sifa kwa Bwana ( Laudato Si,) unaojikita katika mchakato wa kukuchukuliana, kwa upande mwingine inapendekeza jinsi gani nguvu chanya za kihistoria kwa sababu zinatoa ishara kubwa ya muunganiko kati ya nini maana ya kuwa binadamu na kwa upande mwingine, upo ukosefu wa haki na kuonesha ufinyu wa mahusiano kati ya udhaifu wa kibinadamu na mzozo wa ekolojia ya sayari hii. Jibu lake linapatika  katika maendeleo na utafiti wa ekolojia kamili. Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu amependa kusisitiza tena juu ya changamoto za kiuchumi, ambazo zinajikita katika utafiti wa ubora wa mtindo wa maendeleo  wa dhati katika mantiki zaidi ya furaha ya kweli na yenye uwezo wa kusahihisha baadhi ya mifumo inayojitokeza ya utumiaji na uzalishaji. 

Changamoto za Kisiasa:Uwezo wa kiteknolojia unaendelea kupanuka. Moja ya matokeo yake ni kusambaratika kwa utamaduni wa ubaguzi, ambao unameza  mambo ya binadamu bila kubagu;  Uwepo huo unatakiwa kupata elimu ya mtu yenye msingi juu ya mawazo ya binadamu kama mnyang’anyi wa  dunia ambamo anaishi kama njia ya kitega uchumi cha  kupata mali na kujifurahisha mwenyewe. Kazi haikosekani kwa hakika kwa wasomi na watafiti ambao wanashirikiana na Chama cha Mfuko wa Elimu katoliki ( Gravissimum Educationis! Baba Mtakatifu amesema, kazi inaowasubiri kwa msaada wa mipango ya elimu asili  na ili kuweza kuwa makini, lazima kujikita katika mantiki tatu msingi: Hawali ya  yote ni utambulisho. Hii ikiwa na maana ya umakini na kuendelea na utume katika mashule, vyuo vikuu na vituo vya utafiti vilivyo anzishwa, kuhamisishwa au kusindikizwa na Kanisa na kufunguliwa kwa wote. Thamani yake ni msingi ili kuweza kujikita katika mwendo wa ustaarabu wa kikristo na utume wa uinjilishaji wa Kanisa. Kwa njia hiyo wao, wanaweza kuchangia kutoa maelekezo ya njia ya kufuata kwa ajili ya kutoa jibu sahidi dhidi ya kipeo cha kisasa na mtazamo hasa uwaendee  kwa wale wanaohitaji zaidi.

Njia nyingine msingi ni ubora. Hiyo ndiyo taa ya uhakika inayoangaza kila aina ya kuanzisha mafunzo, utafiti na elimu. Hiyo ni muhimu kwa kutimiza kile kiitwacho “ ncha ya hakika, kati ya  maadili” ambayo inasisitizwa na Hati ya Veritatis gaudium (taz n. 5) na ambapo mfuko wa Elimu (Gravissimum Educationis) unachota na kusaidia. Na katika kazi yao, Baba Mtakatifu amewashauri wasikose kuwa na lengo la wema kwa wote. Kwa maana amethibitisha kuwa kuwa na wema wa wote ni mgumu kuulezea  katika jamii ya sasa ambayo inajionesha namna ya kuishi kwa raia, makundi , watu wa tamaduni , kabila na imani tofauti. Ni lazima kupanua upeo wa wema, kuelimisha wote ikiwa ni sehemu moja ya familia ya binadamu.

Mwisho Baba Mtakatifu Francisko amesema, mpango wa mawazo na matendo ambayo tayari yana umuhimu wa misingi hii, unaweza kutoa mchango kwa njia ya elimu, katika katiba na  ujio wa ahadi ya binadamu na undugu duniani ukawa  ndiyo mali ya dunia ambayo kila mzalendo katika dunia hii anaweza kuchota. Baba Mtakatifu Francisko amewashukuru wale wote kwa kile ambacho wanaweza kufanya kwa ajili ya mfuko wao, na kuwatia moyo waendelee katika njia hii yenye sifa na msaada wa utume. Kwa ajili yao na familia zao wamewabariki kwa baraka takatifu ya Bwana na kuwaomba wasali kwa ajili yake.

Na Sr angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.