2018-06-22 14:34:00

kwa mujibu wa UNCTAD na UNECA:Mabadiliko ya miundo ya uchumi inatakiwa Afrika


Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD), na tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Afrika, UNECA daima imekuwa ikisisitiza kwamba ili kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu ya kuimarisha Afrika inahitaji mabadiliko makubwa ya miundo ya uchumi wao. UNCTAD kwa mantiki hiyo wamekaribisha hatua ya tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Afrika, UNECA kujiatiti katika harakati za maendeleo endelevu. Afrika Mashariki ni moja ya kanda inayokua kwa kasi zaidi duniani lakini pia ni mojawapo yenye  nchi maskini. Pamoja na hayo msisitizo juu ya mabadiliko ya miundo hutokea kutokana uelewa zaidi na  kuwa mfano wa ukuaji wa hivi karibuni katika kanda ambazo hazijumuishwi au kujitosheleza.

Mageuzi ya miundo mbinu yamekuwa sehemu ya  sera za kisiasa na inazidi kuchotwa kutoka  katika taarifa za kitaifa na kikanda kwa upeo wa maelekezo kama ya Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Ajenda ya Maendeleo ya Viwanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Hata hivyo,sera zenye makusudi zinahitajika kutekeleza ajenda hizi na hivyo ili  ili kufikia kasi ya mabadiliko ya miundo katika Afrika Mashariki, mawazo ya sera kutoka miili miwili ya Umoja wa Mataifa,  imetoa  nafasi kwa wajumbe,  wakuu wa viongozi wa Umoja wa Mataifa na wataalamu wengine kuchunguza njia za sera za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya miundo katika Afrika Mashariki kwenye mkutano wa siku mbili tarehe 21 - 22 June 2018 katika Jumba la Umoja wa mataifga mjini Geneva, Uswiss.
 
Lengo kuu la tukio la mkutano huo ni kutoa jukwaa la kukuza ufahamu na kujadili jinsi ya kuongeza athari za kiuchumi na maendeleo ya mabadiliko ya kimaumbile. Tukio hili maalum limetafuta zaidi kukuza sera na mikakati jumuishi, kuimarisha mshikamano na ushirikiano na kuongeza msaada kwa juhudi za Afrika ili kuhakikisha mabadiliko ya kiuchumi endelevu katika Afrika Mashariki na barani kote.
Wakati wa mkutano huo Afisa katika ofisi ya UNCTAD, huko Geneva, Uswis, Jane muthumbi akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala la wahamiaji na mambo ya kifiedha ametaja baadhi ya nchi zinazonufaika Barani Afrika ikiwemo Liberia ambayo asilimia 27 ya pato la nchi hutokana na fedha zinazotumwa na wahamiaji. Bi Jane anasema, ingawa wanaishi ughaibuni, wahamiaji bado wanachangia kiuchumi kwenye nchi walizotoka na kwamba nchi  hunufaika, halikadhalika familia zao. Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, imesema fedha zinazotumwa na wahamiaji walioko ughaibuni zimekuwa mkombozi kwa mataifa mengi ya Afrika.  Mathalani kati ya mwaka 2014 na 2016 wahamiaji walioko ughaibuni walituma jumla ya dola bilioni 65 kwa nchi za Afrika. 

Halikadhalika Gambia mwaka jana asilimia 21 ya pato la ndani na Comoro asilimia 20 ya pato la nchi lilitokana na utumwaji wa fedha. Hata hivyo amesema kiwango kinachotumwa kingaliweza kuwa kikubwa zaidi iwapo gharama za kutuma na kupokea fedha kutoka ughaibuni ingalipunguzwa. Kwa hivyo amesema Bi Muthumbi kuwa, hatua muhimu ni kupunguza gharama kwa mujibu wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Na kwa mujibu wa SDGs, gharama hiyo inapaswa kupunguzwa kwa asilimia 3.  http://www.unctad.org/en/pages/MeetingDetails.aspx?meetingid=1868

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News 








All the contents on this site are copyrighted ©.