2018-06-19 14:01:00

Panama iko tayari kuwapokea mahujaji 300,000 toka pande za dunia !


Wakati wa mkutano wa maandalizi ya Siku ya vijana huko Panama, wajumbe wa Baraza la maandalizi mahalia wa Siku ya Vijana Dunia na Baraza la Kanisa Katoliki la Panama, wakiwa na wawakilishi wa Taasisi wamekutana na wawakililishi wajumbe kutoka mabara matano, ili kushirikishana katika mchakato huo wa maadilizi ya Siku ya Vijana Duniani inayotarajiwa kufanyika 2019.

Ilikuwa ni mktano muhimu sana, ambao uliandaliwa vema kwa kuwasaidia wawakilishi wote waweze kujiandaa kikamilifu juu ya  matarajio na wasiwasi wa wawakilishi na mahujaji wengi ambao watatoka pande zote za dunia. Hayo ni maelezo kutoka kwa Padre  Alexandre Awi Mello, Katibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na maisha, aliyechaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo Mei 2017.

Padre Awi Mello alitoa hotuba yake katika mkutano mkuu wa pili wa maandalizi ya kimataifa  huko Panama hivi katibuni kwa ajili ya vijana akiwa pamoja na Kardinali,  Askofu David José Luis Lacunza Maestrojuán, patriaki wa Lisbona  nchini Ureno na Askofu Mkuu José Domingo Ulloa Mendieta wa jimbo Kuu la  Panama.

Wajumbe wawakilishi kutoka mabaraza 80 ya maaskofu duniani, vyama katoliki vya kitume 38, na jumuiya za kimataifa, walio unganika katika mji wa Panama na kukutana na Kamati mahalia ya maandalizi na taasisi ya za maandalizi ili kujadili namna ya kukamilisha tukio tarajio, kushirikisha kwa shauku na matumaini ya vijana katoliki ambao watakutana na Baba Mtakatifu Francisko 2019.

Kwa mujibu wa kamati ya maandalizi mahalia ya Siku ya Vijana duniani, inathibitisha kwamba, Panama iko tayari kuwapokea karibia mahujaji 300,000 ambao wamejiandikisha, kwa kusindikizwa na mapadre na maaskofu, pia karibia watu 5,000 wa kujitolea kimataifa ambao watashirikishana na wengine talanta zao na imani. Sehemu kubwa watatoka nchi za Amerika ya kati na zaidi nchi 9 kati yao tayari wanayo shauku kubwa ya kauli mbiu inayoongoza Siku ya Vijana Duniani: msalaba na picha ya Mama Maria wa Salus Populi Romani, Mama Mlinzi wa watu wa jiji la Roma.

Naye Balozi wa kitume nchini Panama Askofu Mkuu Mirosław Adamczyk, amesema kwa kuzingatia  maandalizi hayo hawali ya yote ni tukio la wokovu hasa akielezea juu ya ushuhuda wa vijana wengi ambao wamegundua upendo wa Mungu mbele ya Msalaba wa Vijana na kwa njia ya Mkutano Mkuu wa Vijana duniani.
 
Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.