2018-06-18 08:46:00

Kanisa Afrika leo hii linajikita na vijana wapate kujitambua !


Kanisa leo  hii  Afrika ndiyo ilikuwa mada ya Mkutano wa Kardinali Laurent Monsegwo Pasinya, Askofu Mkuu wa Kinshasa  nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mmoja kati ya makardinali tisa  washauri wa Baba Mtakatifu Francisko na baadhi ya waandishi wa habari Vatican News katika Ukumbi wa Marcon tarehe 14 Juni 2018.

Kardinali Pasinya amesisitza juu ya changamoto zinazoikumba na zinazoisubiri Afrika Leo hii. Wazo lake la  kwanza limehusu vijana ambao ndiyo wakati endelevu wa bara  hilo na ambao wanaota ndoto ya kupata  ajira, hasa uwezekano wa kupata ajira inayoendana na mafunzo yao. Lakini pamoja na hayo ametoa mifano dhahili kuwa, matatizo siyo machache na kwa maana hiyo amewatia moyo wasiwe na hofu ya kukabiliana , na uwezekano wa mataraji yajayo, lakini akionya kwamba wasije angukia katika mitego ya njia fupi na rushwa. Kutokana na hili amethibitisha kwamba, Kanisa la Afrika lina ujumbe wa kuwapa vijana, ujumbe wa matumaini ya maisha endelevu ambapo lakini wao wanapaswa kuwajibika na kuwa wajasiri wa kukumbatia hata kama inagharimu changamoto mpya na sadaka.

Katika kuelezea nafasi ya  Kanisa katika jamii amesema,  wakati endelevu unapitia kwa njia ya elimu kwani ametoa mifano dhabiti  ya baadhi ya mipango iliyopelekwa  mbele na Kanisa la Angola, Burkina Faso, vile hata katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mahali ambapo amasema , Kinshasa tu kama mji mkuu unahesabu mashule katoliki  590 yakiwemo hata mengine 50 yanayoendeshwa na Parokia na Mashirika ya watawa. 

Na kwa maana hiyo amethibitisha kuwa ni kwa njia ya mafunzo ya elimu kwa vijana wa kizazi kipya kuwa ndiyo njia mwalimu ya kuunda fursa kwa ajili ya kutoa wakati endelevu wa Afrika. Kanisa liko mstari wa mbele kusaidia watu kwa namna ya kushirikishwa, na kutoa kile ambacho kipo. Lakini ni shughuli pia inayojikita hata kwa upande wa afya, msaada wa yatima kutokana na migogoro, vilevile uwezekano wa fursa ya kazi mahali inapowezekana.

Hata hivyo hakukosa pia kelezea juu ya changamoto zinazowakumba vijana, hasa tabia ya kupopendelea kulima mashambani. Amethibitisha jinsi gani vijana walio wengi wanakataa kujiendeleza katika kilimo badala yake wanapenda shughuli za ofisini na mabazo hakuna. Hata hivyo pia ameweza kueleza mada nyingine kama vile ya Baraza la washauri la makardinali, jisni gani ya kusambazwa kwa nyaraka za Kanisa Barani Afrika, mada ambazo zimetokana pia na  baadhi ya maswali ya wandishi. Vilevile juu ya suala la kipeo cha DRC, katika sera za siasa za Rais wa sasa Laurent Kabila. Kwa namna hiyo, ni mategemeo ya Kardinali Pasinya  uwezekano wa  kujikita katika matendo ya dhati katika kuzingatia makubaliano ya mkataba wa tarehe 31 Desemba 2016. Na Kanisa linaendelea kusali kwa ajili ya watu wake ambao wanatamani kwenda mbele tu, kwa maana vurugu na nguvu haviwezi kugeuka mambo ya kawaida.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.