2018-06-18 08:55:00

Inahitaji utandawazi wa mshikamano na uwajibikaji katika dunia hii !


Askofu Mkuu Ivan Jurkovic Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za umoja wa mataifa , ametoa hotuba yake mjini  Geneva kuhusiana na majadiliano ya Global Compact ya wakimbizi na kwamba inahitaji utandawazi wa mshikamano na uwajibikaji wa kushirikisha kama Baba Mtakatifu Francisko anavyozidi kutoa wito kwa viongozi wote wa serikali na waamuzi wengine wa kisiasa, ili kubadilisha kutoka katika utandawazi wa utofauti kuingie utandawazi wa mshikamano, kwa namna ya pekee umakini uwatazame wale wahitaji na waathirika wengi katika familia ya kibinadamu.

Askofu Mkuu pia amesisitiza umuhimu huo wakati wanajadili kuhusu mswada wa Global Compact juu ya wakimbizi ambao ni waraka wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali halisi ya wakimbizi unaopaswa kumalizika na kukubaliwa kufikia mwisho wa mwaka huu 2018. Mabadiliko ya hali halisi ya wakimbizi anathibitisha Askofu Mkuu Jurkovic, yanahitaji mawazo mepesi na vipimo vya kutoa mwelekeo wa  wakati endelevu kwa watu ambao wamelazimka kuacha nchi zao, na kuwasaidia mataifana jumuia ambazo kwa ukarimu wao wanawakaribisha wakimbizi. Kwa njia hiyo Vatican inakubaliana na maono ya waraka huo ambao unalenga kuongeza nguvu ya ushirikiano kimataifa na mshikamano wa dhati kati ya wakimbizi na jumuiya zinazo wapokea kwa njia ya ushirikishwaji wa uwajibikaji sawa  ikiwa na uwezekano wa kuwezeshwa sehemu hizo zinazokaribisha.

Kitovu daima ni kutambuliwa kwa ulinzi na uhamasishwaji wa haki za kibinadamu ili hatimaye  kuweza kuzuia migogoro. Kwa namna ya pekee kwa mtazamo wa kuzuia na kuendesha kesi za matukio, kwa mfano Askofu Mkuu Auza amekumbusha  tabia ile ya kuwabadilisha watu kwa nguvu, na kwamba  siyo suala la bahati mbaya, bali mara nyingi  imekuwa ni matokeo ya maamuzi kisiasa na ukiukwaji wa maono ya vizingiti vya hadhi ya binadamu.

Kwa njia hiyo amebainisha kwamba, Kila mmoja ameunganishwa na kila kitu kimunganishwa, kwa namna hiyo ni muhimu katika Waraka  kuwapo suala la mabadiliko ya hali ya hewa, mmomonyoko wa mazingira, na majanga ya asili ambayo pia yamesababisha  pakubwa wimbi la uhamiaji. Askofu Mkuu Jurkovic amehitimisha akisema ili kukamilisha na kuwa imara ya kupata suluhisho la kudumu ni kuhakikisha haki za wote wanaishi na kutarajia hadhi yao, amani na usalama wa nchi zao mahalia katika nia maalum ile ya elimu, afya na uhamasishaji wa kazi yenye hadhi! 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.