2018-06-12 16:47:00

Kanisa la Korea kusali Novena kwa nchi yao katika kipindi katika kihistoria!


Baraza la Maaskofu nchini Korea wameandaa Novena kwa ajili ya nchi zote mbili, kuombea amani na mkutano wa mapatano, ikiwa pia  kwa ajili ya muungano  watu katika nchi mbili za Korea Kaskazini na Kusini. Ni kufuatia na fursa ya wakati huu ambayo nchi hizi mbili wanakabiliana katika kufungua ukurasa mpya wa kihistoaia na ambayo imewezesha hata mkutano wa viongozi wawili  huko Singapore, Rais Donald Trump na Rais Kim Jong-un wa Korea ya Kaskazini.

Maaskofu katoliki wa Korea wametoa h novena ambayo itaanza tarehe 17 hadi 25  Juni 2018, ambapo kila siku kutakuwa na nia moja moja ya sala wakiomba Mungu kuponyesha  roho za migongano na utengano wa watu wa Korea ; kwa ajili ya familia zilizotengeana kwa  sababu ya vita vya Korea, kwa ajili ya ndugu wanaoishi Korea ya Kaskazini; kwa ajili ya wakimbizi wa asili ya Kaskazini wanaoishi Korea ya Kusini; kwa ajili ya viongozi wa kisiasa wa Kaskazini na Kusini; kwa ajili ya uinjilishaji wa Kaskazini; kwa ajili ya kuhamasisha baadhi ya mabadiliko  na ushirikishwaji kati ya Korea ya Kusini na Kaskazini; kwa ajili ya mapatano kati ya nchi zote mbili ; kwa ajili ya muungano wa amani katika ya Kaskazini na Kusini. 

Tarehe 21 Juni kuanzia saa 8.00 hadi 11 jioni massa ya Korea, utafanyika mkutano katika Seminari Kuu ya katika Kanisa Kuu la Daegu, mkutano unao husu  MAISHA ENDELEVU YA PENINSULA YA KOREA  kwa njia ya mabadilishano kati ya Kusini na Kaskazini. Watakao toa mada ni pamoja na Askofu wa Uijeongbu, Daegu na baadhi ya wataalam.

Hata hivyo tarehe 12 Juni 2018 imethibitishwa kufanyika Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore. Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee wakiwa na wakalimani wao.

Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao. Bw Trump amesema, wawili hao walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano. Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia. Baadaye walitia saini waraka wa makubaliano. Mkutano uliokua ukisubiriwa kwa hamu na ambao umefanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, wanasema mambo makuu manne ambayo Bwana Trum na Kim wameafikiana: Marekani na Korea Kaskazini zitaanzisha uhusiano mpya kati yao,kwa mujibu wa matamanio ya raia wa nchi zote mbili ya kuwa na amani na ustawi;
Marekani na Korea Kaskazini zitashirikiana katika kujenga na kudumisha amani ya kudumu Rasi ya Korea; Kukariri maafikiano ya Panmunjom ya Aprili 27, 2018 wakati wa mkutano wa marais wa Korea Kusini na Kaskazini, kwamba Korea Kaskazini itachukua hatua kuhakikisha kuangamizwa kabisa kwa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea; na  Marekani na Korea Kaskazini zimejitolea kuhakikisha kupatikana kwa mateka wa vita na watu waliotoweka vitani, pamoja na miili yao, ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa wafungwa na miili ya wale waliotambuliwa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.