2018-06-08 11:47:00

Changamo ya Kanisa la Japan mbele ya kufika kwa wahamiaji vijana !


Hali ya hewa mwanana na changamoto ni  vijana wahamiaji kutoka Ufilippini na Vietnam wakiwa na  imani katoliki  ambao wanafika nchini Japan na kushangaa Kanisa la nchi, mahali ambapo wakristo wanawakilishwa asilimia 2% tu ya watu wote nchini Japan. Jamii ya Japan imegeuka kuwa nzee hata jumuiya za kikristo kwa ujumla. Hayo ni maelezo ya Mmisionari padre Ignacio Martinez kutoka nchi ya Mexico anayetoa huduma katika kitengo cha maendeleo ya kijamii ya Baraza la Maaskofu wa Japan kwenye vyombo vya habari katoliki AsiaNews kwa kufafanua tukio ambalo kwa upande wake anaona ni jema la kuongezeka kwa wakristo wahamiaji nchini Japan.

Kwa upande mwingine amesema, kuhusu uzee ni vema kwa sababu wapo watu wengi ambao wamejazwa na uzoefu wa maisha katika nchi hiyo, lakini kwa upande mwingine watu wapya wanaofika kutoka nchi nyingine na sehemu kubwa wakiwa ni wakatoliki na  vijana wanaishi mtindo mwingine na mpya. Hata hivyo, anaendelea kueleza, kwa namna nyingine ni kuwakilisha labda changamoto kubwa hasa  katika parokia zilizo ndogo za vijijini. Akitoa mfano, hivi karibuni alitembelea Parokia moja karibu na Fukushima Kaskazini ya Japan, pale mwanzo kulikuwa na  jumuiya ya watu 20 tu ,na siku moja walifika vijana wafilippini 40 jambo ambalo kwa hakika lilitoa mshangao mkubwa kwa  wajapani.

Maaskofu wa Korea wanao utambuzi wa hali halisi inayoikabili nchi hiyo hasa katika kuongezeka kwa wakristo na wanatafuta kubadili namna ya kufikiria ili kuweza kutenda kwa dhati na kuonesha uhai wa Kanisa katoliki mahalia kama ilivyo duniani. Kati ya mambo hayo Padre Martinez  ametaja, jambo la kuteuliwa Askofu Mkuu Tarcisio Isao Kikuchi, mwaka 2017 kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tokyo, vilevile anaongeza, yeye ni mmisionari wa kwanza aliyefanya utume wake  nchini Ghana barani Afrika, kupewa majukumu makubwa ya kuongoza Jumuiya Katoliki katika Mji Mkuu wa Japan. Askofu mkuu Tarcisio Isao Yama Kikuchi, alikaribishwa na misa kuu mnamo tarehe 16 Desemba katika Kanisa Kuu la Tokyo Japan, kwa uwepo wa maaskofu wote wa Japan, Balozi wa kitume Kardinali  Andrew Yeom Soo-jung, askofu Mkuu wa Seoul , walei kutoka majimbo mbalimbali na mataifa mengine, kama vile nchi za: Corea, Ufilippini na Vietnam hata vijana wengi, pia kuudhuriwa na maaskofu watatu kutoka nchini Ghana, mahali ambapo yeye binafsi alikaa katika nchi hiyo kwa miaka kadhaa akiwa mmisionari pia Balozi wa Ghana nchini humo.

Askofu Mkuu Kikuchi ni mwenye umri wa miaka 60 alizaliwa katika wilaya ya Iwate, na  kuchaguliwa kuwa askofu Mkuu wa Tokyo mwezi Oktoba 2017, pia ni mhusika wa Caritas ya Japan. Nembo yake ya kitume imeandikwa utofauti katika umoja na hivyo ni kuonesha wazi uundaji wa umoja katika tofauti zilizopo katika utamaduni wa Japan kwa neema ya Neno la Mungu! Zaidi Padre Martinez anasema, mwezi Desemba 2017 pia wamempata Askofu  mpya Wayne Berndt, ambaye siyo mjapani bali yeye anatoka nchini Marekani aliyeteuliwa kuongoza jimbo la Naha nchini Japan.

Kadhalika matumaini na furaha ya kufika  wahamiaji katoliki nchini Japan imeweza kuoneshwa na Padre Antonio Camacho Muñoz naye akiwa ni mmisionari kutoka Mexco na mhusika wa maparokia matano katika Jimbo la Kyoto. Yeye methibitisha kwamba, Vijana hawa wahamiaji wanayo imani thabiti na wenye hewa nzuri, mwanana kwa ajili ya Kanisa la Japan. Akifafanua juu ya shughuli zake za parokia amesema, wakati wa maadhimisho ya ibada za misa, wanajitahidi kusoma somo la kwanza kwa lugha ya kivietman na somo la pili lugha ya Kifilippini wakati Injili lugha ya kijapan. Kwa maana hiyo Kanisa lao kwa sasa limeanza kugeuka la Kimataifa. Ni mantiki msingi hasa kwa walio wengi waliozoea kufikiria kuwa nchi ya Japan imejifunga binafsi dhidi ya wageni na kutambua namna ya kukaribisha. Anahitimisha akisema hiyo ndiyo shughuli ya Kanisa Katoliki.

Se Angela Rwezaula 
Vatican News

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.