2018-06-06 15:19:00

Barua ya Kichungaji ya Askofu Mkuu wa Goa kuhusu tatizo la umaskini !


Tatizo la umaskini na sura zake zote ndiyo mtazamo msingi wa barua ya kichungaji  2018-2019 ya Askofu Mkuu Filipe Neri Ferrao wa Jimbo kuu la Goa na Daman nchini India ambapo waraka unatafuta jinsi gani ya kuweza kutoa suluisho la umaskini na sura zake mbalimbali  kama vile kiuchumi na hata zile za kihisia na kiroho.

Waraka wa Kivhungaji pia unajaribu kutoa maelekezo ya mtindo na zana za kutumia ili kupambana kwa ngazi binafsi, kiroho na kijamii. Aidha unaelezea juu ya kuanzishwa kwa shughuli mbalimbali za sasa kwa ngazi ya parokia kati ya vijana. Mapendekezo hayo yote, Askofu Mkuu anasisitiza kuwa yanapaswa kuonekana hawali ya yote upendo Yesu kwa maskini.

Barua hiyo inawalenga mapadre, watawa, kike na kiume, walei na watu wenye mapenzi mema ambao wanaishi katika jimbo kuu hilo. Waraka huo umetangazwawakati wa maadhimisho yaliyoandaliwa katika Kanisa la Mama Yetu wa maskini wa Tilamola.  Katika utangulizi wake, Askofu Mkuu Ferrao anakumbuka kuwa, barua yake ya kichungaji uliyotangulia, mwak 2017-2018 ilikuwa inawaalika wakatoliki na watu wote wenye mapenzi mema umuhimu wa kuwajibikaji kijamii na kuonesha kuridhika kwake kwa namna ambayo Kanisa la Goa lilikuwa limekabiliana na mambo mengi.

Kwa maana hiyo katika Barua ya kichungaji 2018-2019 inaonesha jinsi gani ya kuweze kupunguza umaskini na sura zake, kuanzia kiuchumi na hata ile ya kiroho, ambao unazaliwa kutokana na kukataa, kunyenyekezwa na unyanyasaji, bila kusahau wale ambao wametupwa na jamii kwa sababu nyingine, ukosefu wa elimu, uzee, magonjwa , ukosefu wa ajira, wafungwa na aina mbalimbali za ubaguzi kijamii.

Pamoja na msimamo wa waraka huo kujikita kutazama juu ya kupambana na umaskini katika nchi hiyo, lakini magazeti mengi ya nchini India wao wamejikita zaidi kufikiria mtazamo wa Askofu Mkuu juu ya Kanisa la India akiwaalika wakatoliki wawe mstari wa mbele katika masuala ya kisiasa hasa kwa mtazamo wa uchaguzi mkuu utakao fanyika 2019. Pamoja na hayo lakini,Padre Loila Pereira, Katibu wa Askofu akizungmza na vyombo vya habari, AsiaNews amethibitisha kwamba  Barua ya kichungaji ina kurasa 15 na ambayo kila mwaka husasishwa na Askofu mwenyewe. Na Kauli mbiu inayoongoza barua hiyo ni, Umaskini katika sura zake mbalimbali, kwa maana hiyo katika ya  kurasa 15 neno moja lililotajwa la katiba haliwezi kuwa ndiyo barua ya kichungaji!  

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.