2018-06-04 13:08:00

Waraka wa Baraza la Makanisa duniani uitwao,tunaitwa kubadili matendo!


Shirikisho la Kiluteri duniani na Shirikisho la mshikamano wa matendo na Baraza la Kiekumene la Makanisa watia saini Waraka  uitwao: Tunaitwa kubadili matendo. Ushemasi wa kiekumeni.... Waraka ambao utawakilishwa katika kamati kuu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc) mjini Geneva mapema mwezi huu wa Juni 2018. Ni waraka ambao mashirika matatu yanataka kujikita kwa kina katika uelewa wa ushemasi wa kiekumene na kutoa msingi wa pamoja kwa ajili ya matendo hai  na kutafakari pamoja. Kikundi cha kazi kinaonesha msimamo wa wahusika wa kitaalimungu katika ushemasi na kutoa dira za kujikita katika mantendo kwa wale ambao wanahusika kutoa huduma hiyo. Waraka wenye kurasa 100 unatakiwa kutumiwa kwa ajili ya mafunzo na maenelekezo katika ushemasi wa kiekumene, ili kuongeza uwezo wa taasisi kwa mantiki ya kila mhusika na kusaidia mazungumzo na mshukamano ambao ndiyo hatma ya Makanisa.

Tangu kuanzishwa kwake miaka 70 iliyopita  Baraza la Kiekumene la Makanisa kwa njia ya huduma yake ya kishemasi, imerahisisha kuwashirikisha mamia elfu ya wakimbizi mara baada ya  tukio la vita ya pili duniani. Kwasasa vizazi viwili baadaye, vimeunganisha nguvu zao na kujiunda kwa upya, wakati huo huo na kutoa cheche za ushemasi kwa mantiki ya kazi ya sasa, lakini katika kuelekeza katika mzizi mwingine. Katika waraka pia unasema kwamba, Ushemasi unatafuta njia za kuunganisha duniani, lakini shukrani kwa uhusiano uliopo kati  ya hatua za  uekumene na kujipyaisha na mashirika mengine husika.

Pamoja na kualikwa katika matendo hasa katika kubadilika, Ushemasi wa kiekume una misingi wake  na mzizi kutoka katika mizizi ya maandiko matakatifu ta Biblia, historia, taalimungu na katika kuishi maisha ya sasa ya huduma  hai ya Kanisa. Lengo ni usikivu wa hali ya juu kwa kuweka bayana  kwamba, ushemasi wa kiekumene ni msingi ambao unaweza kujitika katika matendo na kutafakari pamoja katika hatua ya kuelekea umoja kamili ambao ni kwa matashi ya Yesu aliyesema “ili wote wawe na umoja. Kwa njia hiyo, matashi yao ni kuwa, waraka huo unaweza kuwa chombo madhubuti cha kuwasindikiza katika hija ya safari  kwa ajili ya haki na amani ili hatimaye mapenzi ya Bwana yaweze kutilmilizika kwa watu wenye mapenzi mema!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.