2018-05-31 16:16:00

Tarehe 31 Mei ni hitimisho la Mwezi wa Mama Maria kusali Rosari!


Leo hii tarehe 31 Mei ni hitimisho la mwezi wa Mama Maria.  Kila mwaka katika bustani za Vatican kuna maandamano wakiwa wamewasha  mishumaa mikubwa kuanzaia  katika Kanisa la Mtakatifu Stefano wa Abissini hadi kufika  katika Grotto za Mama Maria wa Lourdes.

Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 9 Mei, alikuwa ametoa wito kwa waamini na amahujaji kusali kwa ajili ya nchi ya Siria katika mwezi huu wa Maria. Kwa fursa hiyo Baba Mtakatifu alisema:  kuzeni ibada ya Mama Maria kwa kusali Rosari kila siku kwa kuwa ni mama na  Mama wa Mungu aliyepokea fumbo la Kristo anaweza kuimarika katika maisha yenu ili muweze kuwa na upendo mkuu daima kwa watu wote. .
Na kama ilivyo kwa watangulizi wa mabapa wenzake, hata  Baba Mtakatifu Francisko, ameonesha upendo mkubwa kwa mama Maria. Kwanza tukukimbuka alivyoonesha wazi mara baada ya kuchaguliwa kwake 2013, kwa kumkabidhi Mama maria wa Maria mama wa watu wote katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Rom, pia hata kuwafanya watu duniani, watambue sura ya mama Maria  kama anayefungua mafundo, na tangu wakati huo watu wengi wanasali sala kwa mama Maria anayefungua mafundo…

Sala nyingi za Baba Mtakatifu kwa Mama Maria  zimefanyika hata kww mfano wa sala kwa  Mama Maria Mkingiwa wa dhambi ya Asili katika uwanja wa Uhispania Roma kila tarehe 8 ya Desemba yak ila mwaka, mahali ambapo Baba Mtakatifu amesisitiza kuhusiana juu ya msaada wa mama Maria anaoutoa kwa watu wote, ili kuweza kushinda matatizo ya maisha. Ni mara ngapi Baba Mtakatifu pia katika mahubiri yake ameweza kumtakma Mama Maria , haua  kwenye sikuu ya Picha ya Mama Maria wa watu Wote Roma, mwezi Januari 2018,alisema kuwa: moyo ni bahari ya dhoruba, mahali ambapo mawimbi mazito ya matatizo yanakusanyika juu yake na pepo za mahangaiko haziishi kamwe kuvuma na kupuliza kwa nhvu na hivyo Mama Maria ni safina ya hakika katika gharika kuu, na mabaye tunaweza kukimbilia.

Wakati anahitimisha mwezi wa Maria 2013, kwenye  sala ya Rosari, Baba Mtakatifu alisali sala hii: Maria mama msikivu, atusaidie kusikiliza atusaidei kubaki masiki yetu wazi; atusaidie kumbua kusikiliza Neno la Mwanaye Yesu Kristo kati ya maelfu ya maneno ya dunia; atufanye kusikiliza  hali halisi tunayoishi, na kila mtu tunaye kutana naye, hasa wale maskini, wahitaji na wenye matatizo. Maria mama wa maamuzi, atuangaze akili na roho, ili tuweze kutii Neno la Mwanaye Yesu Kristo bila kusita; atupatie ujasiri katika maamuzi na hasituache tuchuliwe na mambo ili kuondokana na mwelekeo mwema wa maisha yetu. Maria mama wa matendo, atusaidie ili mikono yetu na miguu yetu iweze kuanza kutembea kwenda kwa haraka kwa wengine ili kupeleka msaada na upendo wa Mwanao Yesu Kristo, kwa sababu ya kupeleka kama yeye mwanga wa Injili duniani!

Na sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.