2018-05-30 16:21:00

Papa Francisko ayataka Makanisa kutembea kwa pamoja!


Tarehe 30 Mei 2018 kabla ya Katekesi, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wawakilishi wa Upatriaki wa kiorthodox kutoka Moscow, Urusi ambapo wakati wa mazungumzo yake bila kuandika amewashukuru kwa ujio wao na mkutano huo ambao unawafanya waendelee kuishi imani yao katika umoja na matumaini ya kutembea pamoja.  Anayo furaha ya kutembea kwa pamoja katika mchakato  wa njia inayotoa ahadi ya kitu cha uhakika kwa sababu njia ya mgawanyiko uleta vita na uharibifu. Mbele yao na mbele ya Kanisa amethibitisha kwamba, Kanisa Katoliki, haliruhusu kamwe pazaliwe matendo ya migawanyiko.Kwa maana hakuna tena nafasi ya tabia hiyo kamwe!

Aidha amesema kuwa huko Moscow nchini Urusi kuna Patriaki mmoja na kwa maana hiyo hatambui mwingine zaidi ya huyo. Amebainisha kwamba inapojitokeza mwamini katoliki,awe mlei, padre,askofu kuchukua bendera isiyo ya umoja na ambayo haifanyi kazi tena, ina maana ya kumtia  uchungu kwa upande wa Baba Mtakatifu!  Ni lazima kuheshimu makanisa ambayo yameungaza na Roma, lakini ukosefu wa muungano kama hatua ya umoja, leo hii haina nafasi, Baba Mtakatifu amethibitisha, vile vile kwamba, faraja yake ipo katika kuona mikono inayofunguliwa, mikono ya kindugu na  ambao wanafikiria kutembea pamoja. 

Njia ya uekumene inafanyika ikiwa katika hatua za safari ya pamoja. Japokuwa amebainisha kwamba wapo wengine wanaofikiria kuwa hilo siyo haki na kwamba mwazo ni lazima pawepo makubaliano katika  mafundisho, kwa kutazama vipengele vyote venye kuleta mgawanyiko na ndiyo kuweza kutambea pamoja. Lakini kwa mujibu wa Baba Mtakatifu anasema, uekumene wa namna hiyo hauwezi kufanyika hivyo kwa sababu haijulikani ni siku ipi itakuwa ya makubaliano. Ametoa mfano mmoja kuwa, alisikia mtu mmoja wa Kanisa na  mtu wa  Mungu akisema, mimi ninajua siku ambayoitawekwa sahini ya makubaliano ya mafundisho ya Kanisa . Na alipoulizwa lini akajibu,“ Siku ya kuja kwa utukufu wa  Kristo. 

Baba Mtakatifu ameongeza kusema:  tunalazimika kuendelea kusoma taalimungu  ili kuhakikisha kila aina ya hatua hiyo, lakini wakati huo huo tukiwa tunatembea pamoja, ndiyo maana hakuna haja ya kusubiri ili kutatua mambo kama  hayo na kama kizingiti cha kutotembea pamoja.  Ni kutembea kwa pamoja katika ukweli na upendo, katika sala, ya kuombeana mmoja na mwingine na vilevile kuwa na mazungumzo. Baba Mtakatifu Pia amekumbuka mkutano na Patriaki Cyrill na kuthibitisha kwamba: katika mkutano huo  alijisikia vizuri kukutana na ndugu yake huyo, hadi sasa wanatembea pamoja kiroho.

Kwa kuhitimisha maneno yake bila kuandika, Baba Mtakatifu ametoa maneno mawili: moja juu ya heshima ya wakatoliki mbele yao ndugu wa kiorthodox wa Urusi, kwamba: Kanisa, Makanisa Katoliki wasijichanganye katika mambo ya ndani ya Kanisa la Kiorthodox la Urusi, ikiwa hata mambo ya kisiasa. Na ndiyo mtindo wa Vatican leo hii. Kwa maana wale wanao jichanganya hawatii Vatican kwa upande wa Kisiasa.  Na jambo la pili ni huruma: Kwa upande huo, Baba Mtakatifu Francisko amekazia umuhimu wa sala kwa ajili ya kutembea pamoja, lakini pia sala binafsi kwa maana upo  utambuzi wa ndugu kaka na dada wapya. Kwa maana hiyo, anatoa mfano: alipokutana na Patriaki, baadaye alimtumia masalia ya Mtakatifu Serafin na masalia hayo anasema yapo katika meza yake. Kila usiku kabla ya kulala na asubuhi anapoamka anasali kwa ajili ya umoja. Kwa njia hiyo amemalizia akiwataka  kuombeana mmoja na mwangine na kuwabariki kwa baraka takatifu wakati huo akirudia kwa upya kuhimiza juu ya kutembea kwa pamoja.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.