2018-05-28 15:03:00

Papa Francisko ameeleza umuhimu wa utume wa kimisionari wa Kanisa!


Baba Mtakatifu Francisko, ametuma ujumbe wake kwa njia ya Video kwa ajili ya shughuli ya kipapa za kimisionari,(POM) kufuatia ufunguzi wa Mkutano wao mkuu wa mwaka, tarehe 28 Mei 2018. Baba Mtakatifu katika ujumbe huo anaonesha shauku kubwa ya kutuma ujumbe huo kwa njia ya video ili kuonesha kwa dhati hali halisi na umuhimu wa utume wa Kanisa ambao kwa dhati anasisitiza kuwa unajulikana kidogo yani utume wa kipapa wa kimisionari.

Akiendelea na ufafanuzi amesema,tangu mwanzo wa husaidizi wa pamoja kati ya Kanisa mahalia linalojikita katika kutangaza na kushuhudia Injili, shughuli hiyo imekuwa ishara ya Kanisa ulimwelinguni. Kwa hakika umisionari ambao unaongozwa na Roho wa Bwana Mfufuka, unapanua nafasi ya imani na upendo hadi miisho ya dunia.

Katika Karne ya XIX, utangazaji wa Kristo uliotoa uhai mpya kwa kuundwa wa Kazi ya Kimisionari, kwa lengo maalum hasa ya  kusali na matendo ya dhati ili kusaidia kazi za  uinjilishaji katika maeneo mapya. Shughuli hizo zilitambuliwa na Papa Pio XI ambaye alipenda kusisitizia juu ya utume wa Kanisa kuelekea kwa watu wote ambao walikuwa moyoni mwa mfuasi wa Mtakatifu Petro. Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu anasema, hata sasa, shughuli za kimisionari za kipapa zinaendelea kuwa muhimu hata leo hii. Huduma hiyo ilianza karibia miaka 200 iliyopita na ambayo ipo katika nchin 120 zikiongozwa na Wakurugenzi Kitaifa  na undeshawaji wa Sektratarieti ya Kimataifa  iliyopo Vatican.

Je ni kwanini ni muhimu shughuli za kimisionari za kipapa ? Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, hawali ya yote ni lazima kusali kwa ajili ya wamisionari wote na kwa ajili ya matendo ya uinjilishaji wa Kanisa. Sala ndiyo shughuli ya kwanza ya kazi ya kimisionari, ambapo kila mkristo anapaswa kufanya, japokuwa anathibitisha, kwa dhati kwamba siyo rahisi kupima.  Lakini zaidi uya hayo  shughuli hizo zinawakilisha   jina la Papa katika ugawanaji sawa wa msaada, ikiwa na maana ya makanisa yote duniani ili kuweza  kusadiwa hata kile kidogo,  kama vile uinjililishaji, kwa ajili ya sakramenti , kwa ajili ya mapadre wazalendo, waseminari, kwa ajili ya kazi ya kichungaji na makateksta. Kuwasaidia wamisionari wanao injilisha hasa zaidi kwa ajili ya msaaada wa sala na kwa njia ya Roho Mtakatifu azidi kuwa hai katika maisha ya Kanisa. Na ndiyo yeye anapeleka mbele shughuli ya uinjilishaji!

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anawatia moyo wote ili  kushirikiana  pamoja katika  shughuli ya kutangaza Injili na kusaidia Vijana ambao wanajikita katika shughuli za kimisionari. Kwa kufanya hivyo kila mtu na  Kanisa wataendelea kujifungua kwa wote na kutangaza kwa furaha Habari Njema ya Yesu Kristo, mkombozi wa dunia.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News.








All the contents on this site are copyrighted ©.