2018-05-25 17:12:00

Mh. Padre Ernest Obodo ateuliwa kuwa Askofu msaidizi Jimbo la Enugu


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Ernest Obodo kutoka Jimbo Katoliki la Enugu, nchini Nigeria, kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki Enugu. Askofu mteule alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1966 huko Awha-Imezi, Jimboni Enugu. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, kunako tarehe 22 Julai 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo, katika maisha na utume wake kama Padre amewahi kuwa: Paroko-usu, Paroko, Mlezi Seminari ya Mt. Bernard, Nchatancha na baadaye akateuliwa kuwa Katibu Jimbo.

Amewahi kuwa Mlezi wa Jumuiya ya Mtakatifu Yuda na mwanachama wa Tume ya Historia, Jimbo Katoliki Enugu. Kati ya mwaka 2010 hadi mwaka 2016 alipelekwa na Jimbo kuendelea na masomo ya juu na kubahatika kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Innsbruck, kilichoko nchini Austria. Kuanzia mwaka 2016 akateuliwa kuwa Gombera wa Seminari kuu ya Mt. Bernard na Jaalimu katika Seminari ya Kumbu kumbu ya Bigard, iliyoko Enugu, nchini Nigeria.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.