2018-05-22 12:59:00

Hija ya Masalia ya Mtakatifu Yohane XXIII huko Bergamo alikozaliwa!


Masalia ya Mtakatifu Papa Yohane XXIII yatasafirishwa hivi karibuni kwenda  mjini Bergamo  Italia Kaskazini, mahali alipozaliwa. Tukio hili la kipekee litaanzia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Masalia ya Papa Yohane XXIII yaliyoko mbele ya kaburi la Mtakatifu Petro yaliamishwa kutoka kwenye Groto za Vatican mnamo mwaka 2001, mwaka ambao alitangazwa kuwa mwenye heri.
  
Kardinali Angelo Conastri, Askofu Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ametoa tafakari fupi kwa njia ya video, Habari za Vatican News, kuhusiana na sura na hija ya masalia ya Papa huyo. Masalia ya Mtakatifu Yohane XXIII yatakuwa huko Bergamo chini ya mlima kuanzia tarehe 24 Mei hadi 10 Juni 2018, mahali ambapo waamini tayari wanasubiri kupokea masalia hayo kwa furaha kubwa.

Hili ni tukio maalum na ambalo liliwahi kutokea mnamo mwaka1960, mahali ambapo masalia ya Mtakatifu Pio X aliyerudi huko aliko zaliwa Venezia nchini Italia, kwa utashi ya Papa huyo huyo  Yohane XXIII. Kardinali Comastri anaongeza: pamoja na hayo tukio hili linatoa fursa ya kutafakari kwa kina urithi wa Papa huyo  katika Mtaguso wa Pili na  ule wa “Pacem in Terris” yaani  Amani duniani. Kwa mujibu historia na maelezo ya mwaka 1958 baada ya uchaguzi wake ambao ulimchagua kuwa kharifa wa Mtume Petro, wanasema, utume wake kama kipapa ulikuwa ni wa mpito.

Kardinali Comastri anakumbuka pia jinsi gani mizizi yake na familia yake ilicyokuwa ni nyenye nguvuz sana na hasa   hisia za lugha yake rahisi aliyo kuwa anatumia na kueleweka kwa wote. Kwa namna hiyo Kardinali anathibitisha kwamba, anaamini  lengo la  Papa Yohane XXIII anayetazama yote akiwa juu mbinguni anaweza kuwa anasema, “endeleeni kuhifadhi ile chemichemi ambayo mimi nilichota, mahali ambapo mimi niliiga katika maisha yangu”. Hata hivyo Kardinali Comastri ameeleza vilevile juu ya kutangazwa kwake kuwa Mtakatifu, iliyofanyika mnamo mwaka 2014 kwa njia ya Baba Mtakatifu Francisko na kwamba alimtangaza Mtakatifu bila ya kusubiri hata muujiza wa pili. Kwa maana ya mantiki ya kutambua fadhila za kiajabu za moyo wa Papa Yohane wa XXIII na zile za moyo wa Yesu.

Na Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.