2018-05-21 16:01:00

Askofu mkuu Marek Zalewski ateuliwa kuwa Balozi Singapore na Vietnam


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Marek Zalewski kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Singapore na atakuwa pia Balozi wa Vatican asiye na makazi nchini Vietnam. Kabla ya uteuzi huu,  Askofu mkuu Marek Zalewski alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa tarehe 2 Februari 1963 huko Augustow, Jimbo Katoliki la Lomza, nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 27 Mei 1989.

Tarehe 25 Machi 2014 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe na hatimaye, kuwekwa wakfu hapo tarehe 31 Mei 2014. Ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Alianza kutoa huduma za kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 1995 na kupangiwa huko: Jamhuri ya Afrika ya kati, Umoja wa Mataifa, Uingereza, Ujerumani, Thailand, Singapore na Malaysia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.