2018-05-18 17:07:00

Ujumbe wa Baraza la Mazungumzo ya kidini katika fursa ya mfungo wa Ramadhan


Katika fursa ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, umetolewa ujumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini ukiwa na kauli mbiu “wakristo na waislam: kutoka katika mashindano kuelekea ushirikiano  kwa ajili ya mwezi wa Ramadhan na ‘ID AL-FITR 1439 H. / 2018 A.D.

Ujumbe huo umetiwa saini na Karidinali Jean-Louis Cardinale Tauran Mwenyekiti wa Baraza hilo na Katibu Mkuu Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot, M.C.C.J. Katika ujumbe  unasema kuwa katika ukarimu wa Mwenyezi aliyewapa uwezekano wa kuanza kwa upya mfungo wa Ramadhan na ili wapate kusheherekea ‘Id al-Fitr,  Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini linatambua umuhimu wa mwezi huo  pia juhudi kubwa kwa upande wa waislam wote duniani kufunga, kusali na kushirikishana zawadi za Mwenyezi kwa watu walio maskini zaidi.

Katika utambuzi wa zawadi zitokanazo na Ramadhan, wanaungana pamoja kumshukuru Mungu wa huruma kwa wema na ukarimu wake na kuwatakia matashi mema. Katika ujumbe huo, pia wanaonesha lengo pia la kutaka kushirishana juu ya mantiki ya mahusiano ya wakaristo na waislam kwamba, upo ulazima wa kuachia mbali michakato ya mashindano na  ili kuelekea katika ushirikiano. Hiyo ni kutokana na kwamba mahusiano kati ya wakristo na walislam kwa miaka mingi imepitia mara nyingi katika roho ya mashindano, ambayo matokeo yake yanaonekana kuwa hasi, kwa mfano wa wivu, ubaguzi na mivutano. 

Kutokana na masuala haya yamezalisha zaidi hata vurugu nyingi na zaidi kuleta uhasi wa dini ambayo imetaka kutumia kwa ajili ya manufaa binafsi kwa upande hata katika vyama vya kisiasa. Matokeo hasi ya kidini wakati mwingine yameleta sura nyingine ya dini kwa mfano wa wale  wafuasi wao kuongeza mawazo ambayo siyo kisima cha amani, kinyume wamezalisha  mivutano na vurugu.

Kwa njia hiyo Viongozi wa wa Baraza hili wanathibitisha kuwa  ili kuweza kushinda matokeo hasi ni muhimu wakristo na waislam pamoja na kutambua tofauti zilizopo, na wakati huo kujikita zaidi pamoja kutafuta thamani za dini hizo kwa kile kinachoungaisha zaidi  ya kile kinachotengenisha. Kutambua kila mbacho tunashirikishana zaidi na kuonesha heshima kwa kila aina ya utofauti huo, ndipo tunaweza kweli kusimama na imani thabiti katika  mahusiano ya amani,na kuacha nyuma  mashindano na vurugu kwa kusisitizaia juu ya ushirikiano wa kweli kwa ajili ya wema wa pamoja.  Na hiyo itasaidia zaidi kuleta faida kwa wale wanahitjai zaidi na kwa pamoja kuweza kutoa ushuhuda wa kuaminika wa upendo wa Mwenyezi kwa ajili ya binadamu wote.

Ujumbe unahitimishwa ksema: “Sisi wote tunayo haki na wajibu wa kutoa ushuhuda wa Mwenyezi ambaye sisi tunafanya ibada na kushirikishana imani zetu kwa wengine, katika kuheshimu dini na hisia za dini za wengine”. Kwa maana hiyo ili kuweza kutia moyo katika mahusiano ya amani na kidugu, ni lazima kufanya kazi pamoja kusifu na kubadilishana uzoefu. Kwa njia hiyo tunaweza kutoa sifa kwa Mwenyezi na kuhamasisha umoja katika jamiii ambayo daima inazidi kuongeza kabila, dini nyingi na utamaduni nyingi.  Ujumbe unarudia kwa upya upya kutoa matashi mema kwa ajili ya matunda ya mfungo utakaofuata sikukuu ya  Id  Mbarakha kwa kuwahakikishia mshikamano wao katika sala.
 
Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.