Waraka mpya wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Baraza la Kipapa
la Maendeleo endelevu ya Binadamu umepewa jina la “Oeconomicae et pecuniariae quaestiones”
ambao una kusanya mawazo kwa ajili ya mang’amuzi ya maadili katika baadhi ya mantiki
ya sasa kwenye mfumo wa uchumi na fedha. Na katika utangulizi ambao unaelekeza Waraka
huo mpya wa “Oeconomicae et pecuniariae quaestiones, wanaandika kuwa “Dhana ya kiuchumi
na fedha kwa ajili ya maendeleo katika njia ya ustawi wa binadamu uwe halisi na endelevu.
Inapaswa kufungamana wazi katika msingi wa maadili na lazima kuonekana kati ya ufahamu
kiufundi na hekima ya binadamu”.
Waraka huo umekubaliwa na Baba Mtakatifu Francisko na kutangazwa kwa wote. Pamoja
na kutangzwa umewakilishwa kwa vyombo vya habari Vatican na Kardinali Peter Turkison
Baraza la Kipapa la Maendeleo endelevu ya Binadanadamu pamoja na Kardinali Ladaria,
Mwenyekiti wa Barza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa . Katika waraka huo, unaonesha
vipengele mbalimbali msingi kama vilivyo fafanuliwa kwa kirefu kama vile: Upendo wa
wema kamili ni ufunguo wa maendeleo; ulimwengu unaotawaliwa na mantiki zilizokwisha
wakati; kuchuma na kufaidika binafsi ni maombolezo; uchumi na utamaduni wa ubaguzi;
tabia za ubinafsi zinafanya kulipa gharama kubwa kwa wote; mitindo mipya ya uchumi
na hatimaye kipengele cha mwisho ni kile cha kutafuta wema wa pamoja.
Upendo wa wema kamili ni ufunguo wa maendeleo: Katika kujikita kwenye Wosia wa
Laudato Si wa Papa Francisko, Waraka huu wanasititiza kuwa, upendo wa jamii na juhudi
za kutafuta wema wa pamoja zinaundwa kwa mtindo wa upendo ambao hautazami tu mahusiano
kati ya mtu, badala yake ni mahiusiano ya ulimwengu, mahusiano ya kijamii, kiuchumi
na kisiasa.Ufunguo wa maendeleo ya dhati ni upendo wa wema wa pamoja ambao hauteni
na upendo kwa ajili ya ukweli.
Na ili kuweza kuhamasisha maendeleo hayo ni ngumu hasa kwa upande wa mang’amauzi
ya kimaadili. Na Kanisa linatambua kati ya kazi yake msingi ambayo inawaalika wote
kwa unyenyekevu wa uhakika katika baadhi ya mantiki msingi
Ulimwengu unaotawaliwa na mantiki zilizokwisha wakati wake: Katika Waraka mpya unatathimini
pia hata historia ya hivi karibuni ambayo inajikita katika uchumi duniani. Kipeo
cha sasa cha fedha , kingeweza kuwa fursa ya maendeleo na uchumi mpya zaidi katika
umakini wa maandili msingi na katika utaratibu mpya wa kuratibu shughuli za fedha
kwa kuyeyusha zile mantiki ya wizi na uchunguzi wakati hyo huo kuweza kuthaminisha
zaidi huduma ya uchumi wa sasa. Lakini pamoja na juhudi chanya katika ngazi mbalimbali
kwa bahati mbaya umekosekana uhusiano mwema na ukaleta matokeo yaliyofikia kufikiria
mantiki ambazo zinaendelea hadi sasa kutawala dunia!
Kuchuma na kufaidika binafsi ni maombolezo:Matukio ambayo hayakubariki ni yale ambayo yanatokana na kuchuma na kunyonya vilevile kuendelea kunufaika binafsi na kujitajirisha pasipo kufaidisha wengine, kwa maana hiyo ni kuunda wasiwasi katika ustawi wa walio wachache au wakati wakati mwingine uchumi unatawaliwa na kushushwa bei ziweze chini na ambazo zinasabaisha kupanda kwa madeni mengi ambayo yanawakilisha matokeo hasi katika hali halis ya nchi nyingi.
Uchumi na utamaduni wa ubaguzi: Pamoja na hayo hata wasiwasi juu ya mantiki ya
uchumi ndiyo Papa Francisko anaitafsiri, “utamaduni wa ubaguzi” Katika Waraka unathibitisha
kuwa, ni mchezo wa kweli wa ustawi watu katika sehemu kubwa ya watu wanaolia katika
sayari hi ina ambao wako hatarini, wameachwa pembezoni mwa jamii bila kuwa na maendeleo
yoyote kwasababu ya kunyonywa malighafi na utajiri wote ardhini mwao.
Ubinafsi unafafanya kulipa wote gharama kubwa: KatikaWaraka huo inaonesha ulazima
wa kufikiria kwa upya mitindo ya uchumi kutokana na ukosefu wa kugawana sawa. Kwa
maana hiyo wanasema imewadia sasa wakati wa kufikiria kwa dhati kibindamu na kupanua
upeo wa akili na moyo, kwa kuwa na utambuzi wa hali halisi kwa kile kinacho fikia
katika dharua ya kweli na wema.
Mitindo mipya ya uchumi: Wataalamu na wahusika wanaalikwa kwa namana ya pekee kushirikiana katika mitindo mipya ya kiuchumi na fedha mahali ambapo mchakato na utaratibu viweze kuweka katika maendeleo endelevu kwa wote, kuheshimu hadhi ya binadamu, uhakika wa zana za mafundisho jamii ya Kanisa. Hata hivyo hata ule ulazima wa kuanza kwa upya kutafakari juu ya mantiki za kuwa wawakili wa fedha ambao unatambua kusimamia na kufanya kazi kwa maana mara baada ya kutenguka kwa msingi ya maadili na maandili ya binadamu ndiyo unasababisha matokeo ya ukosefu wa haki sawa vile vile kuonekana kwa mfumo mbaya ulio undwa ana ambao unazidi kutmika duniani.
Kutafuta wema wa pamoja: Ili kuweza kuratibu vema mifumo ya sasa ya kiuchumi na
fedha, kila mmoja anaweza kufanya mambo mengi sana, hasa iwapo hakuna ubianfsi na
kujitenga kwa maana vipo vyama vingi vya kiraia ambavyo vinawakilisha kwa maana nyingine,
utunzaji wa dhamiri njema na uwajibikaji kijamii. Leo hii kama zamani, waraka unahitimishwa
na kusisitiza kila mmoja anaalikwa kuwa makini kukesha kama walinzi wa maisha bora
na kutafsiri kwa upya wakiwa mstari wa mbele kijamii katika matendo haid na thabiti
kutafuta wema wa pamoja ambao unajikita katika misingi imara ya mshikamano na kugawanya
wa usawa wa pamoja
Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©. |