2018-05-11 15:21:00

Cei:Mitandao ya kijamii isaidie kutoa habari njema katika jamii !


Hivi karibuni  wakati wa kozi kwa wakurugenzi wa mawasiliano kitaifa wa Baraza la Maskofu  Italia, Padre Ivan Maffeis Mkurugenzi wa Ofisi ya kitaifa ya Mawasiliano wa CEI, ameweza kuonesha  nyenzo zote zinazo tumika katika mawasiliano kwa upande wa Baraza na  ambapo amesisitizia juu ya vyanzo hivyo kama vile  Sir, kituo cha matangazo ya Radio InBlu, Televisheni  (Tv 2000) na  Gazeti la Avvenire vikiwa ndiyo mama wa vingine vingi vipya.

Akifafanua zaidi amesema, nyenzo hizi ni wazo rahisi ambalo linatoa nafasi kuu ya kutoa vyanzo vya habari za kweli na zilizo kusudiwa kwa ajili ya wema katika jamii. Na uwepo wa vyombo hivi una maana sana kwa sababu ni kwa mara ya kwanza, wameweza kufanya mawasiliano ya Kanisa katika mitandao ya kijamii kwa  umoja. Yote hayo ni kutaka kufungua dirisha la mazungumzo kwa watu wote, ikiwa ni kutoa thamani na utajiri wa matokeo ya vyombo vya habari walivyo navyo ndani ya Kanisa katika ulimwengu.

Hata hivyo katika dhana ya sasa, Kanisa la Italia pia limo ndani ya mfuno wa kisasa wa  moja kwa moja katika mikondo ya mitandao ya kijamii ambap inapatikana kwa njia ya Facebook, Twitter na  YouTube, laki pia hata zille mpya katika mitandao ya dunia kama vile, Paper.li, Spreaker, Spark. Na zaidi ni raihisi kwa watumiaji wote wa  kufuatia katika Computa, smartphone na tablet,  habari za moja kwa moja katika vipindi vya Kanisa kupitia kituo cha Televisheni  ya Italia (RAI katika kipindi cha “Sua immagine”  na  Televisheni ya Maaskofu Italia “Tv2000” kwenye matukio yote muhimu ya Kanisa la Italia.

Askofu Nunzio Galantino, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wakati wa hotuba ya kufunga kozi hiyo Laterano Roma, amesema kuwa, ni jambo jema na kufurahisha iwapo unaweza kugundua nafasi ya chachu kwa upande wa waamini katika mitandao ya kujamii. Ni chachu iwapo kuna mapendekezo ya kutumia muda wao na nguvu zao kutafuta mahusiano ya kweli na kutoa nafasi ya kuuliza maswali halisi zaidi badala ya kuridhika na jibu lisilo sahihi na lenye  uhakika kama wafanyavyo walio wengi mtandao kwa halama ya ( like ) yaani “napenda” .

Akifafanua juu ya chachu, anathibitisha kwamba, huwezi kuitunga chachu na kuiwezesha binafsi iwe kubwa, maana ni yenyewe peke yake inafanya kazi ndani yake na kujikuza, mfano huo huo anaufanisha na  picha ya utamaduni ndani ya jamii na kwamba upo uwezekano wa kukua maono mapya ya binadamu ambayo wakati mwingine yamedharauliwa ndani ya maono hayo ya kibinadamu. Lakini ni lazima kuwa na utambuzi ya kuwa, chachu inakua ndani ya ulimwengu bila kuwa na utukutu wa kujipendelea binafsi badala yake ni kuwa na furaha hasa kwa yule anayehisi kuitwa na kuhudumia Injili na siyo kutumikishwa na Injili!

Aidha katika hotuba yake, Askofu Galantino amejikita zaidi kutazama kiini cha mkutano wao  mkuu wa maaskofu wa Italia utakao fanyika, hasa katika swali la kuulizia nafasi ya Kanisa  ya sasa kwa mantiki ya mawasiliano. Ili kuelezea zaidi juu ya Mkutano mkuu, amethibitisha kuwa, lengo kuu si kujihusisha zaidi na suala la zana gani  zitumike katika Kanisa la Italia katika  mawasiliano ya sasa na mantiki zake, au  kiini cha tafakari hakitagusia  hata jinsi gani ya kuweka nguvu ya kuona  ukuu wa nyakati hizi za vyombo vya mawasiliano, badala yake lenzo kuu ni kujikita kutazama kwa kina ni  jinsi gani Kanisa linakuwa na dhamiri kwa ujumla kutazama  Kanisa leo hii linavyokazana  kutangaza na kuelimisha Injili iliyo njema. Ni muhimu kuwa na dhamiri kamili ambauo ni kiini cha kuendeleza mikondo mingine ya mawasiliana na kujiuliza maswali ya kukabiliana changamoto zilizokuwapo na zile ambazo zipo katika mantiki mpya ya mawasiliano.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu anasema,  jamii ya mawasiliano siyo tu kuelezea au namna, bali ni kufikia hali halisi ya kuunda au kutengeneza uhalisia wa utambulisho wa mtu pia kukua katika utambuzi wa kuchukua wajibu katika  nafasi chanya ambayo inakuwezesha kushika nafasi ya nguvu na ambayo inakualika kwenda kutangaza habari iliyo njema!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.