2018-05-05 14:15:00

Vumbi kutimka katika Kilele cha Miaka 50 ya Njia ya Ukatekumeni Mpya Roma!


Ni furaha kubwa kukutana nanyi leo hii, asante Mungu hata ninyi pia, zaidi kwa wale waliosafiri safari ndefu ili kuwepo hapa; asante kusema ndiyo kwa kuitikia wito wa Bwana wa kuishi Kiinjili na kuinjilisha. Asante sana hata walio anzisha Njia ya Ukatekumeni Mpya kwa miaka 50 iliyopita! Haya ni  maneno ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko aliyo anza nayo asubuhi ya tarehe 5 Mei 2018 kwa wanachama cha Kitume cha Njia ya Ukatekumeni Mpya kutoka pande  mbalimbali za dunia, waliofika Roma ili kukaa na Baba Mtakatifu Francisko na kumwimbia Mungu wimbo wa shukrani, Te Deum , wakiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa utume wa chama hicho.

Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Tor Vergata Roma, maarufu sana kwa  miaka 18 iliyopita, kwani ndiko waliadhimisha Siku ya Vijana Duniani mwaka 2000, sanjari  na Jubilei ya Ukatoliki. Katika maadhimisho hayo, Baba Mtakatifu Francisko amewabariki na kuwatuma mapadre 35 wa Chama cha Njia ya  Wakatekumene Wapya kwenda katika utume duniani, vile vile familia 25 kwenda katika maparokia mbalimbali ya pembezoni mwa mjini Roma.

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake amesema, miaka 50 ni muhimu katika maandiko matakatifu; kwa maana  inaonesha kuwa, siku hamsini Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume Kanisa likajionesha duniani. Lakini kabla ya hiyo,  Mungu alikuwa amewaonesha mwaka wa hamsini na kuubariki na kusema, “ kwa kuwa  Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni wa sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini; msipande mbegu, wala msivune kitu kiotacho chenyewe, wala kuchuma  zabibu kutoka miti msiyoipogoa”(taz Walawi 25,11). Ni Mwaka Mtakatifu ambao watu wateule wangegusa kwa mikono yao hali halsi mpya, kama vile ya  kukombolewa na kurudi makwao, kwa maana  Bwana alikuwa amesema: “Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini na kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake”.

Baba Mtakatifu anaendelea, tazama baada ya miaka 50  katika njia  hiyo ,ingekuwa vizuri kila mmoja akasema, asante Bwana kwa kuwa umenikomboa kweli na kwa sababu ndani ya Kanisa nimepa familia; kwa sababu ya ubatizo, mambo ya zamani yamepita na sasa yapo mapya ; (taz 2 Cor 5,17); na kwa  njia hii umenielekeza njia ya kugundua upendo wako mtamu Baba. Halikadhalika Baba Mtakatifu akielezea juu ya utenzi wa Te Duem ambao umeimbwa kushukuru upendo na uaminifu wa Mungu, amethibitisha kwamba, ni vizuri sana kushukuru Mungu kwa upendo wake na uaminifu ma daima tunamshukuru kwa zawadi zake, kwa kile anacho tujalia. Lakini zaidi ni kumshukuru kwa jinsi  tulivyo, kwa sababu Mungu ni mwaminifu katika upendo wake. Na wingi wa upendo huo hautegemei na nguvu zetu sisi au kile tunacho kifanya, kwa maana yeye anaendelea kutupenda kwa uaminifu wake. na kwa manaa hiyo  Yeye ndiye kisima cha matumaini yetu na faraja ya maisha.

Anawatia moyo wasichoke  kamwe na kukata tamaa pale wanapo kumbana na matatizo ambayo kwa wakati mwingine ni mazito kila siku, lakini kutokana na hilo wakumbuke daima kuwa,upendo wa Mungu ni mwaminifu na jua lisizame kamwe bila kuwa na shukrani. Kadhalika wajitahidi kila wakati kufanya  kumbu kumbu ya wema aliowajalia,zaidi ya mabaya waliyo tenda, kwa maana ni utamu wa kukumbuka upendo wa Mungu ambaye anawasaidia  kwa kila ngazi ya maisha yao.

Akiwageukia wale ambao wanakwenda katika utume wa kimisonari anasema:Unjilishaji ndiyo moyo wa Kanisa leo hii, kwa sababu, utume ni kutoa sauti ya upendo mwaminifu wa Mungu na kutangaza kuwa, Bwana anawapenda wote, hachoki kamwe kuwaita katika dunia hii, badala yake ni watu  wenyewe wanaomchoka Mungu. Kwa maana hiyo baba Mtakatifu amesema, utume ni kutoa kile ambacho tulicho nacho. Utume ni kutimiza agizo la Yesu ambalo limesikika katika Injili ya Mtakatifu Matayo akisema: "endeneni duniani kote  mkawafanye kuwa wafuasi wangu" (Mt 28,19). Aidha Baba Mtakatifu anasema jambo la kwenda katika utume linakulazimu uondokea,  japokuwa katika maisha kuna vizingiti vinavyokubana na hasa, kuna vishawishi vya nguvu ambavyo vinakuzuia usiondoke anasisitiza Baba Mtakatifu na kuongeza ni vishawishi ambavyo vinakufanya usitake kujiingiza katika hatari, vile vya kuridhika na hali uliyo nayo na  ili uweze kuithibiti kila kitu kinacho kuzunguka!

Halikadhalika amesema, ni rahisi kubaki umezungukwa na wale wanao kutakia mema, wakati huo huo hiyo si njia ya Yesu! Kwa maana Yeye anaagiza  kuondoka, bila kuwa na kifaa chochote. Kwa njia hiyo ni wito wa nguvu kwa wakristo kuweza kujisadaka na kuwa msafiri katika dunia hii, ili kutafuta ndugu ambaye bado hajatambua furaha ya upendo wa Mungu. Lakini je ni jinsi gani ya kwenda? Baba Mtakatifu mejibu kuwa ni Injili aliyo wakabidhi. Biblia inafundisha kuwa, Mungu alipo wakomboa watu wateule, aliwafanya watembee katika jangwa wakiwa na sanduku moja tu, yaani tumaini moja kwake. Kwa  kutembea wakiwa maskini na bila kuwa na mahali pa kujiegemeza kichwa (taz Lk 9,58). Huo ndiyo mtindo wa wafuasi wake  ili waweze kwenda katika kazi ya umisionari kutangaza Neno lae na lazima kujikana binafsi.

Baba Mtakatifu amesema, Bwana mfufuka aliwambia mitume wake, wakawafanye mataifa yote kuwa wafuasi wake, lakini  hakuwaeleza wakawanunue na kuwatawala, bali wawe wafuasi, ikiwa na maana ya kushirikishana na wengine, zawadi waliyo ipokea na  kukutana na upendo ambao ni wa kubadilishana katika maisha. Moyo wa umisionari ni kushuhudia kwamba, Mungu anawapenda na kutokana na hili upendo wa kweli upo, ambao unasaidia kujisadaka kwa wengine kila mahali unapokuwa iwe katika familia, kazini; uwe mtawa  au mwenye ndoa, Baba Mtakatifu anathibitisha!

Umisionari ni kurudi kuwa wanafunzi wapya wa Yesu,ili  kugundua kwa upya njia ya kufanya  sehemu ya mtume wa Kanisa.  Kwa dhati Kanisa ni mwalimu, lakini haiwezi kufanya mwalimu iwapo haikuwa kwanza  mwanafunzi, kama jinsi ilivyo kwamba, huwezi kuwa mama kabla ya kuwa  mtoto na ndiyo maana tazameni yupo Mama. Kwa maana  Kanisa ni la  unyenyekevu na mwana wa Baba, mwanafunzi na Mwalimu wake  ambapo wote wanakuwa  na furaha ya kuwa na dada ambaye ni binadamu. Ndiyo dhana ya kuwa mfuasi, pia mfuasi  kuwa mtume, ni to rofauti ya mantiki ya upropaganda!

Halikadhalika Baba Mtakatifu anafafanua kuwa, Nendeni Duniani kote na kuwa mwanafunzi wangu: Yesu alipotamka hayo utafikiri alikuwa nasisitiza zaidi  kuonesha kuwa katika moyo wake kuna nafasi ya kila mtu. Hakuna anayebaguliwa. Kama ilivyo wana kwa baba na mama, hata kama ni wadogo na wakubwa, lakini kila mmoja amependwa kwa moyo wote.  Kwa sababu katika kutoa upendo, haupunguzi bali upendo huo unaongezeka. Na ndiyo daima matumaini. katika hilo, Baba Mtakatifu Francisko ametoa mfano mmoja juu ya Upendo wa Mungu kwetu ya kwamba, mara nyingi ni kama vile wazazi wengi wasio ona kasoro za watoto wao;wanaona  watoto wao tu na kuwapokea jinis walivyo katika mwanga, hata kama wana matatizo.

Hawatangulizi kuona kasoro katika mioyo ya watoto wao, bali ule wema na ndiyo Mungu anavyotazama kila mmoja, wema uliopo ndani ya kila mtu. Kwa kufikiria hilo, Mungu anavyopenda dunia hadi kumtoa mwanae, wanachama cha Njia ya Ukatekumene,  wawe na shauku ya kupenda ubinadamu, kushirikiana kwa furaha na wote, kuwasikiliza na kuwa karibu kwa wote. Wapende utamaduni na mila na desturi za watu, bila kuwaingizia mitindo mipya. Wasisafiri na unadharia au mipango iliyokwisha kamilika badala yake wajikite  katika hali halisi kushirikiana nao, maana yupo Roho Mtakatiti ambaye atatangaza kwa mujibu wa nyakati na mtindo wake. Hiyo ni kutokana na kwamba Kanisa likuza sura yake ya umoja katika utofauti wa watu, zawadi na karama nyingi, amesisitiza Baba Mtakatifu

Amehitimisha kwa kusema: karama yao ni zawadi ya Mungu kwa ajili ya Kanisa katika nyakati hizi, kwa maana hiyo, anamshukuru Mungu kwa miaka 50, akiwatazama kwa upendo wake na uaminifu huo, anawashauri wasikose  kuwa na matumaini kamwe. Kwa maana yeye atawalinda na kuwasaidia wakati huo huo, waendelee mbele  kama mitume, wapende watu wote, waoneshe unyenyekevu na wawe rahisi. Anawasindikiza kwa sala  na kuwatia moyo waendelee mbele!

Sr Angela  Rwezaula 
Vatican News!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.