2018-05-04 16:54:00

Papa Francisko amekutana na Kikosi cha Ulinzi cha Uswiss na familia zao!


Tarehe 4 Mei 2018 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Kikosi cha Kipapa cha  Ulinzi na Usalama cha Uswiss mjini Vatican na wageni wao kufuatia na fursa ya kupata kiapo chao kama walinzi wa kharifa wa mtume Petro.  Katika hotuba yake, amewakaribisha wote kwa namna ya pekee kikundi cha vikosi vya ulinzi na familia na marafiki wao ambao wamependa kushiriki katika sikukuu yao kwa siku hizi. Aidha amewapa salama hata wawakilishi wa madaraka kutoka nchini Uswis ambao pia wamefika katika afla hiyo.
 
Akiwageukia wanajeshi anasema, wao ni wenye uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa kipindi watakachokuwa mjini Roma, ili kuweza kufanya uzoefu wa aina yake katika chuo kikuu cha Kanisa. Muda huo unaweza kuwa fursa  kwao na kuwatia nguvu katika imani ya kukua kwa maana ya kushiriki kikamilifu katika jumuiya ya kikristo.  Shughuli yao inajikita kabisa kwa ujasiri na uaminifu wa papa ambapo ilianzishwa  mnamo tarehe  6 Mei 1527 ambapo walinzi kutoka Uswiss walitoa maisha yao kwa ajili ya kulinda Kanisa na Baba Mtakatifu. 

Akifafanua juu ya shughuli ya kikosi cha kipapa  cha ulinzi na usalama kutoka Uswiss kinachojikita katika shughuli  za kila siku mjini Vatican Baba Mtakatifu amesema, ni kikosi  cha Ulinzi wa Kipapa ambacho kina dhamana na kuendelea kushuhudia ule utulivu na furaha kwa wale wote wanaofika mjini Vatican ili kutembelea Kanisa kuu la Mtakatifu Petro au kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Kharifa wa Mtakatifu Petro, kwa namana hiyo anawapa  mwaliko wa kuwa imara na thabiti katika imani, na kuwa wakarimu wenye upendo wa dhati kwa wote wanaokutana nao!
  
Vilevile akiedelea na kueleza juu ya shughuli  kikosi hiki tangu mwanzo kama mashujaa ametoa mwaliko kwa wote kuendelea kuonesha thamani hiyo hiyo kwa amani na na msimamo wa imani katoliki; utimilifu na urafiki na Yesu  upendo kwa ajili ya Kanisa ; kuwa na furaha katika shughuli zao zikiwa kubwa au ndogo za unyenyekevu kila siku.  Ujasiri na uvumilivu, ukarimu na mshikamano na wote, Baba Mtakatifu anasema ndizo fadhila ambazo wao wanaalikwa kuzifanyia mazoezi watakapokuwa wanatoa huduma yao kwa ajili ya ulinzi na usalama mjini Vatican, hata wakiwa nje ya mavazi yao. Kikosi cha Ulinzi na usalama kutoka Uswiss, daima kinajulikana hivyo, wawe ndani ya huduma na hata wakiwa nje ya huduma hiyo, Baba Mtakatifu anathibitisha.

Ni vizuri kuona kijana kama wao anaonesha umakini kwa wengine na uwezekaoa wa kusaidia wale ambao wanahitaji. Hiyo ni kwasababu Baba Mtakatifu anaongeza, siyo rahisi daima kutoa ushuhuda katika tabia ya namna hiyo, lakini kwa msaada wa Bwana inawezakana! Na zaidi Baba Mtakatifu anawaomba wasichoke kukutana na Bwana Yesu katika sala ya Jumuiya na binafsi, kusikiliza kwa makini Neno la Mungu na kushiriki kikamilifu Ekaristi Takatifu.

Siri ya kazi yao Vatican, hata katika mipangpo yao ya maisha inategemea zaidi kukutana na Kristo. Baba Mtakatifu pia anatumia fursa hiyo kurudia kwa upya, kuwashukuu Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha Papa kutoka Uswiss. Anawapongeza kwa adabu yao  hasa wakati wa kutoa huduma yao na kuonesha taaluma yao katika huduma hiyo na zaidi ule utulivu wanao uonesha kila siku wakati wa huduma mjini Vatican.

Anamshukuru Mungu kwa zawadi nyingi ambazo anawajalia kila mmoja na kuwaombea  ili waweza kuimarika na kuzaa zaidi matunda. Na kwa njia ya maombi ya Bikira Maria ambaye anakimbiliwa katika mwezi wake wa Rosari na watakatifu wasimamizi wawalinde. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amewapa Baraka ya kitume kwa ajili ya ndugu jamaa na marafiki, hata kwa ajili ya nchi yao! 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.