Tarehe 5 Mei 2017 Njia ya Ukatekumeni Mpya unafanya mkutano mkubwa wa kimataifa huko Tor vergata jijini Roma na Baba Mtakatifu Francisko katika furaha ya maadhimisho ya miaka 50 tangu chama hicho kikanyage mguu wake Roma, mara baada ya kuanzishwa mjini Madrid nchini Uhispania mwishoni mwa mwaka 60. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu atawabariki na kuwatuma wanajumuiya 34 ya ""Missio ad gentes na Jumuiya 25 za chama hicho katika umisionari kwenye parokia za pembezoni mjini Roma. Mkutano na Baba Mtakatifu Francisko utaanza saa 5 masaa ya Ulaya lakini saa 4 kamili wataanza na utangulizi kutoka kwa Kiko Argüello, mwanzilishi wa kimataifa katika hatua hizo cha chama cha kitume cha wakatekumeni wapya.
Eneo lilochanguliwa kufanyika mkutano ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Tor Vergata,
kando ya mji wa Roma kwa ajili ya kumuenzi Mtakatifu Yohane Pauli II ambaye kwa miaka
26 kama Khalifa wa mtume Petro aliwakaribisha na kuwasaidia mchakato wa hatua za chama
hiki cha kitume cha wakatekumeni wapya. Na ikumbukwe, Tor Vergata ndiyo mahali ambapo
waliadhimisha Siku ya Vijana duniani Mwaka 2000 ikiwa ni Jubilei ya Ukristo ! Kutokana
na maombi ya maaskofu wengi, mitume wapya amvao ni mapadre 34 wa missio ad gentes
wataweza kubarikiwa na kutumwa ili wapeleke Injili katika maeneo mengi yaliyomezwa
na malimwengu au sehemu ndogo ya uwepo wa Kanisa katika miji duniani kote.
Baba Mtakatifu pia atawabariki na kuwatuma jumuya 25 za wakatekumeni wapya katika
maparokia ya Roma ambao tayari wamefanya hatua za mchakato wa hatua za ukristo,
hata katika parokia nyingine pembezoni mwa Roma, mahali ambapo maparoko wameomba msaada
ili kusaidia wengi ambao wako mbali na imani. Mkutano wao utahitimishwa na sala ya
wa shukrani, “Te Deum”, ikiwa na maana ya kushukuru Mungu kwa miaka 50 tangu kufika
mjini Roma chama cha kitume hiki. Maombi ya shukrani yataongozwa na kikundi cha kimataifa
cha wakatekumeni wapya. Pamoja na hayo watamkumbuka kwa namna ya pekee hata Carmen
Hernández, mwanzilishi msaidizi mwenzake wa Kiko wa chama cha Kitume cha wakatekumeni
wapya aliyerudi kwa baba mbinguni mnamo tarehe 19 Julai 2016.
Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©. |