2018-05-03 13:59:00

Kuonesha imani siyo kufanya propaganda bali ni upendo na ushuhuda!


Kuonesha imani, siyo kufanya propaganda, kama vile kutafuta washabiki wa michezo au kama ilivyo katika kituo cha utamaduni, badala yake kuonesha imani ni kushuhudia kwa upendo. Ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko aliyofanya wakati wa Misa Takatifu katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican tarehe 3 Mei 2018 wakati Mama Kanisa anafanya kumbukumbu ya watakatifu mitume Filipo na Yakobo.

Tafakari ya Baba Mtakatifu imeanzia katika Somo la Mtakatifu Paulo kwa Wakorinto, na kuweka bayana juu ya tabia ambazo mkristo anapaswa kupeleka na kuonesha imani yake na kwamba, imani siyo tu kusali sala ya Nasadiki, badala yake ni kuitafsiri katika matendo.

Kupeleka imani haina maana ya kutoa maelekezo badala yake ni kujiundia ndani ya moyo wako katika imani na Yesu Kristo. Ni jambo mabao liko mbali kabisa na kuchukua kitabu au aina nyingine, kuwa mkristo maana yake ni kuzaa matunda wa kuplekea na kuonesha imani hiyo, kwa maana hiyo ni kama Kanisa ambalo ni Mama na linazaa watoto wake katika imani.

Baba Mtakatifu amesisitiza zaidi juu ya kupeleka na kurithisha imani katika kizazi endelevu na kwamba, ni kuanzia kwa bibi hadi mama, katika hali ya kutoa  manukato ya upendo. Imani binafsi inasafiri, si kwa njia ya  maneno tu, bali kwa njia ya kubembeleza na kuwa na upendo hadi kuongea hata lugha ya kuzaliwa. Katika maneno ya Papa  Francisko ndipo yamepata hata nafasi kwa upande wa watu wanao tunza wazee na ambao amesema ni mama wa pili.  Hao wawe mgeni au la, wamezidi kuongezeka na ambao wanaonesha imani yao wakitunza na kusaidia imani hiyo ikue.

Kwa njia hiyo tabia ya kwanza ya kurithisha imani kwa hakika ni upendo, wakati huo huo tabia ya pili ni ile ya kushuhudia. Papa Francisko anaendelea: Kurithisha imani siyo kufanya propaganda, badala yake ni kitu kingine na kikubwa zaidi. Kwa maana hiyo si tabia ya kutafuta washabiki wa michezo, wa club fulani au katika kituo cha utamaduni; kwa upande huo sawa inawezekana, lakini kwa upande wa imani hatufanyi propaganda. Imani inasambazwa hawali ya yote kwa mvutio wa kupendezwa yaani kwa njia ya ushuhuda.

Kishuhudia katika maisha ya wote ya kila siku na ambayo yantufanya tuwe wenye haki mbele ya macho ya Mungu ni udadisi kwa wale wanao kuzunguka. Ushuhuda unazaa udadisi ndani ya moyo wa mtu mwingine na udadisi huo anauchukua Roho Mtakatifu na kwenda katika kazi ndani yake. Kanisa linaaminika kwa mvutio na kukua kwa uvutio. Kurithisha imani unatokana na ushuhda hadi kifodini anathibitisha Baba Mtakatifu. Hiyo ni kutokana na muonekano wa maisha na ndipo unazaa udadisi kwa mfano: je kwanini huyo anaishi hivi? Kwanini katika maisha anajikita katika kuhudumia wengine?

Kutokana na udadisi huo ndiyo mbegu ambayo Roho Mtakatifu anaichukua na kuipanda na kuipeleka mbele. Na ndiyo  kuonesha na kurithisha imani inayotufanya tuwe wenye haki mbele ya Mungu. Imani inatupatia haki na katika kuridhisia imani hiyo tunatoa haki ya kweli kwa wengine!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.