2018-05-02 16:00:00

Papa Francisko kuanza mwezi wa Rosari katika Madhabahu ya Divino Amore !


Kama alivyo kuwa ametangaza, Baba Mtakatifu taarifa kuhusu siku ya  Mei Mosi  mchana kuazana mwezi wa Bikira Maria kwa kutembelea Madhabahu ya Bikira Maria huko “Divino Amore” kando ya mji wa Roma kuungana na waumini wengine kusali Rosari kwa namna ya pekee kwa ajili ya nchi ya Siria na Dunia nzima, amehitimisha hija hiyo jioni ya Mei Mosi! “Tusali kwa pamoja kwa ajili ya amani nchini Siria” ndiyo wito wa Papa Francisko aliowaomba maelfu ya waamini waliofika katika Madhabahu ya mama Maria wa Divino Amore, Roma. 

Ni maelfu ya waroma waliompokea Papa Francisko katika uwanja mbele ya Mnara wa Muujiza wa kwanza katika Madhabahu ya Mama Maria wa Divino amore, dakika chache kabla ya kufika saa 11 majira ya jioni masaa ya Ulaya. Baba Mtakatifu amechangua mwaka huu kuanza mwezi wa Maria kwa hija  katika madhabahu inayopendwa sana na watu wakazi wa Roma. Kabla ya kuingia katika Madhabahu ya zamani ili kusali Rosari Takatifu, amewasalimi waamini waliokuwa wamekusanyika katika uwanja na kuwomba wamfuatile  wakiwa pale kusali Rosari.
  
Wakati akiingia  katika madhabahu ya zamani mbele ya Picha ya Mama Maria wa miujiza, msomaji alikuwa akiendelea kusoma wito wa amani kwa ajili ya nchi ya Siria. Ni maneno yaliyo tamkaBaba Mtakatifu wakati Sikukuu ya Pasaka, kama utamaduni wa kutoa baraka ya Urb et orbi  mbele ya Kanisa la Mtakatifu Petro Mjini Vatican.

Pamoja na waamini wote ambao tayari walipata nafasi katika Madhaahu ndogo ya zamani, wamesalia rosari ya matendo ya uchungu. Baada ya Sala ya Rosari, Baba Mtakatifu amerudi kiwanjani mahali ambapo maelfu ya watu walikuwa wakimsubiri na ambao wamesali naye wakiwa kwa nje. Na kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amesali Sala ya Salam Maria na baadaye kuwabariki na kuanza safari ya kurudi Vatican.
 
Ziara ya Baba Mtakatifu siku ya Mei Mosi katika Madhabahu ya Bikira Maria wa Divino Amore, imesindikizwa na Askofu Mkuu Angelo de Donatis, makamu mkuu Askofu wa Roma, Askofu Paulo Lojudice Msaidizi wa kitengo cha Roma kusini, Monsinyo Enrico Feroci , Mkuu wa Shirika la Waoblati wa Wana wa Mungu Upendo, Padre Luciano Chagas, Gombera wa Madhabahu hiyo, Padre Vincent Pallippadam Gombera wa Seminari ya Maria wa Divino Amore na Paroko  Padre John Harry Bermeo Sanchez.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.