2018-04-30 15:56:00

Papa Fracisko amekutana na wawakilishi wa wanachama wa Maisha Hadimu!


Rafiki wapendwa asante kufika kwenu! Asante Mwenyekiti Baba David ambaye amesimulia historia yen una hata tendo la kuwaleta hapa Roma kwa ishala ya Matumaini. Daima ninafurahi kukutana na vyama kwa ajili ajili ya utafiti na mshikamano juu ya magonjwa hadimu. Kwa hakika kuna uchungu kwa ajili ya mateso na kazi ngumu lakini ambayo daima inanishangaza na kubaki na butwaa kwa mapenzi ya wanafamilia wanao jikita pamoja kukabiliana na hali halisi, kwa kufanya kila iwezekavyo kuboresha. Ninayo Giorge na Rosita pamoja na David, mtoto wenu, mlisukumwa kwa ndani utashi wa kufanya lolote kwa ajili yake na wengine ambao wanateseka na magonjwa adimu na kwa ajili ya familia zao.

Ni maneno ya hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi tarehe 30 Aprili 2018, wakati alipokutana na wanachama cha “Maisha hadimu”, mjini Vatican. Chama cha Maisha hadimu ni chama kisichokuwa cha kiserikali ambacho kina malengo ya kutafuta kila hali uwezekano na mshikamano wa kijamii kwa ajili ya kusaidia utafiti wa kisayansi na kulinda afya wakati huo huo kutoa matibabu ya Magonjwa hadimu, ambayo kwa dhati yanahitahiji umakini (Allan-Herndon-Dudley Syndrome AHDS-MCT8)  kuchelewa ukuaji wa ubongo; mishipa ambayo husasabisha viungo kutofanya kazi yake vizuri na mtindio wa akili.

Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake amesema, jina la Chama chao kiitwacho Maisha hadimu, kinaeleza hali halisi ya David, lakini hata pia maisha yao, ambapo ni kwa namna chanya na siyo hasi. U hasi upo unatambulikana  kwa hali halisi ya kila siku, lakini kwa jina hilo lenye utambuzi  wa kutazama uchanya, ya kwamba kila maisha ya mwanadamu ni ya pekee, hata kama ugonjwa ni adimu au nadra sana, lakini kabla ya kuwezekana ni uwepo wa maisha yake.

Mtazamo huo chanya, ndiyo mtindo wa kawaida wa muujiza wa upendo. Upendo unafanya hivyo kwa maana unajua kutazama wema hata katika hali halisi ambayo nihasi, upendo unatazama kutunza cheche ndogo ya moto katikati ya giza nene la usiku. Upendo unafanya muujiza, maana unasaidia kubaki umefunguka kwa ajili ya wengine; kuwa na uwezo wa kushirikishana, kuwa na mshikamano hata ukiwa unateseka na ugonjwa au katika hali nzito na uchovu wa kila siku.

Baba Mtakatifu Francisko anaamini ya kuwa, mtindo kama huo ni kumshukuru Mungu Mungu  kwa kuanzishwa kwa njia ya mbio za kilometa 700,  katika mchezo mbio zilizoanzishwa siku kumi zilizopita kuanzia katika nyumba yao hadi kufika Roma. Na mnio kwa ajili ya maisha na kwa ajili ya matumaini. Kwa maana hiyo anawapongeza wote ambao wameweza kutoa maisha hayo wakiongozwa na kauli mbiu
 “Mbio za Maneno hadimu” na kwa wote walioshirikiana. Amehitimisha na shukrani tena na kuahidi maombi yake, lakini pia wao wasimsahau katika sala zao.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.