2018-04-30 15:22:00

Baba Mtakatifu ametoa onyo juu ya udadisi zaidi katika mitandao ya kijamii!


Watoto wana udadisi sana na hata katika dunia ya mitandao wanakutana na mambo mabaya sana. Ni lazima kuwasaidia vijana wasiwe wafungwa katika udadisi huo, badala yake kuomba nguvu ya Roho Mtakatifu anayetoa uhakika. Ndiyo wazo kuu la Baba Mtakatifu Francisko aliotoa asubuhi ya tarehe 30 Aprili 2018, wakati wa mahubiri yake katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Kutambua namna ya kung’mua kati ya udadisi mwema na ule mbaya na kujufungulia Roho Mtakatifu anayetoa uhakika, ndiyo wito wa Baba Mtakatifu Francisko ambapo amweza kutafakari wakati wa Misa ya siku, kwa kuongozwa na Injili ya ya  Mtakatifu Yohane (Yh 14,21-26) inayohusu mazungumzo kati ya Yesu na mitume wake. Baba Mtakatifu anathibitisha kwa kufafanua ya kuwa yanahusu  mazungumzo kati ya udadisi na uhakika. 

Udadisi mwema katika umri wa kwanini: Akielezea  juu ya utofauti kati ya udadisi mwema na ule mbaya anasema, hiyo ni kwasababu katika maisha yetu yamejaa udadisi. Kwa mfano udadisi mwema kama ule wa watoto ambao kwa kawaida  unaitwa umri wa kuuliza ni kwa nini. Swali hilo linakuja kutokana na kwamba, kadiri mtoto anavyozidi kukua ndivyo maswali yanajitokeza, maana uwepo wa mambo mengi asiyo yajua, hivyo watoto wanatafuta maelezo na ufafanuzi kamili. Huo ndiyo udadisi mwema, kwa maana unakuza ili kuwaweza kujitegemea pia ni udadisi wa kutafakari kwasababu watoto wanatazama, wanatafakari na wasipoelewa wanauliza!

Umakini katika mazungumzo na dunia ya mitandao: Simulizi nyingi ni udadisi mwema, urithi wa wanawake na wanaume hata kama kuna wengine wanasema kuwa, wanaume wanaongea sana zaidi ya wanawake. Lakini udadisi mbaya ni ule wa kutaka kunusa maisha mengine zaidi, hasa ya kutaka kutafuta kwenda katika nafasi ambazo mwishowe zinachafua nafasi za watu wengine, kwa kutaka kutambua mambo ambayo huna haki ya kujua. Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, mtindo wa udadisi huo mbaya unatusindikiza katika maisha yetu yote ; kwa maana ni kishawishi ambacho tutakuwa nacho daima. Pamoja na hayo nasema, hakuna kuogopa japokuwa ni lazima kuwa makini, kwa maana ya kusema sitauliza kitu,  sitazami hilo, na spendi hilo. Aidha kuna hata udadisi mwingine kwa mfano katika  mitandao ya kijamii, simu za mikono na mambo mengine, ambapo watoto wanakwenda pale pale  na wana udadisi wa kutaka kutazama, lakini  wakati huo huo wanakutana na mambo mengi mabaya. Hakuna nidhamu katika udadisi huo. Tunapaswa kuwasaidia watoto kuishi katika ulimwengu huu, kwa sababu hamu ya kujua siyo tamaa ya kuwa na udadisi,  na ambayo inafanya kuishia kuwa wafungwa wa udadisi huo.

Roho Mtakatifu anatoa uhakika:Udadisi wa mitume katika Injili ni mwema, kwa maana wao walitaka kujua ni kitu gani kitatukia. Yesu alijibu na  kuwapa uhakika na kamwe  hakuwadanya, na kuahidi Roho Mtakatifu ya kwamba, atawafundisha kila kitu na kuwakumbusha yote aliyowaleza. Uhakika tunapewa na Roho Mtakatifu katika maisha. Lakini Roho Mtakatifu haji kwa kawadia kama ufikap mzigo wa posta na ukauchukua. Badala yake ni katika kipimo ambacho sisi tunaomba katika maisha hasa  kuomba Roho Mtakatifu atufungue mioyo, na kwa hakika  anatupatia muda huo, yaani jibu la maombi kwa wakati huo. Kwa njia hiyo Roho Mtakatifu ni msindikizaji katika maisha ya mkristo. Roho Mtakatifu anatukumbusha maneno ya Bwana na kutuangazia katika mazungumzo mezani akiwa na mitume wake, na mazungumzo hayo ni udadisi wa kibinadamu na uhakika ambao unaishia kugusia Roho Mtakatifu huyo, ambaye ni msindikizaji wa kumbukumbu inayotufikia katika furaha ya kweli ambayo haitingishiki.

Baba Mtakatifu amewaalika waamini wote waende mahali ambapo kuna furaha ya kweli na Roho Mtakatifu anayesaidia kutopoteza njia. Amehitimisha akiomba Bwana mambo mawili leo hii, kwanza kutusafisha kukubali udadisi lakini ambao ni mwema na siyo ule mbaya ili kuweza kutambua kung’amua. Pili ni kuomba neema ya kufungulia mioyo yetu Roho Mtakatifu ili kuwa na uhakika wake yeye, maana anatupatia uhakika, kama msindikizaji katika safari yetu kwenye mambo ambayo Yesu mwenyewe ametufundisha na kutukumbusha.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.