2018-04-27 15:42:00

Mshikamano wa Vijana katoliki nchini Malawi wasaidia familia hitaji!


Mshikamano wa wakristo kwa ajili ya wenye shida na walio wa mwisho katika jamii daima unazidi kujizatiti kwa dhati katika nchi maskini kama Malawi, mahali ambapo chama katoliki cha vijana wafanyakazi (Young catholic workers (Ycw), wa jimbo Kuu la Blantyre hivi karibuni  wameweza kutoa zawadi ya nyumba kwa familia moja maskini katika kijiji cha Mulanje.  Familia hiyo siyo katoliki  lakini ambayo ndani yake kuna mama mzee na mtoto wake akiwa na watoto 6, kati ya watoto hao ni mgonjwa wa ubongo,  ambaye alitambuliwa tangu mwaka  2015 kwa njia ya mpango wa matibabu na matunzo mbadala. Mpango wa Chama hicho kinajihusisha kusaidia kuhamasisha  na kuendeleza huduma ya kutunza kwa njia ya matunzo mbadala kwa wagonjwa na familia za  wa Blantyre na jumuiya zinazoizungukia.

Padre Chrispin Ngunde, rais mstaafu wa chama cha vijana wafanyakazi (Ycw) akielezea katika shirika la habari katoliki Fides anasema, kwa kuongozwa na kauli mbiu yao ya “ tazama, hukumu na tenda, iliwasaidia kuingilia kati suala hili la familia iliyokuwa inahitaji ya mambo msingi  kabla ya yale ya lazima. Hata kama familia hiyo haikuwa katoliki anasisitiza, wao wameweza kutoa zawadi ya nyumba ya kuishi.

Wakati wa sherehe za kukabidhi nyumba hiyo,mwenyekiti wa kijiji alishukuru Vijana katoliki kwa mfano wa kazi hiyo waliyotenda  hata kuwaalika wanakijiji kuiga mfano kama huo. Kwa mshangao mkubwa anasema, hasingeweza kamwe kufikiria kile ambacho kimetukia katika kijiji hicho. Na hivyo hana maneno ya kueleza zaidi kwasababu familia hiyo umepata matumaini kutokana na kuishi kwa taabu zao.

Na mmoja wa wanafamilia wakati wa kushukuru hawali ya yote ametoa shukrani kwa Mungu kwa baraka waliyoipokea na kwamba ni kama ndoto ambayo wasingefikiria kati ya familia nyingi za kusaidia katika kijiji lakini kuchagua wao, kwa maana hiyo ameomba mwenyezi Mungu kwa niaba ya wana familia ili aweza kuwabariki wao na hata Kanisa zima Katoliki kwa mshikamano hai kwa wale wenye kuwa na matatizo.

Aidha hata Padre wa Parokia cha Chisitu huko Mulanje ametoa shukrani ya dhati kwa zawadi hiyuo na kuzidi kuwatia vijana waendelee na shukghuli zao katika shula kwa namna ya mendeleo endevo na wawe mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya katika jumuiya zao. Aidha amweao,ba hata vijana wengine katika vijiji vao, kuiga mfano wa chama cha vijana wafanyakazi katoliki ambao wameonesha kuwa wainjilishaji wema wa matendo hai.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.