2018-04-27 16:28:00

Maaskofu wa Chad wanataka ifanyike kura ya maoni katika kubadiki Katiba!


Inahitajika kura ya maoni  ili kubadilisha Katiba,ndiyo maelezo ya Waraka wa Baraza la Maaskofu nchini Chad walio utoa katika mkutano wao mwaka. Tarehe 30 Aprili 2018 kutafanyika Mkutano wa Kitaifa  nchini Chad ili kuweza kupiga kura kuhusiana na makubaliano ya mpango wa mageuzi ya katiba, ambayo haikukubaliwa na wapinzani,katika  Baraza la Mawaziri,mnamo tarehe 10 Aprili 2018.

Kati ya masuala yaliyoleta mgogoro zaidi ni kuhusu kuongezeka muda wa utawala wa urais kutoka miaka 5 hadi 6 na kuongezeka kwa madaraka ya Mkuu wa nchi.Wapinzana wanathibitisha kuwa, Katiba iliyokuwa imewekwa ni ile ya kutaka kusaidia rais Rais Idiriss Derby Itno andelee kuwa madarakani milele, lakini  Katiba moja ambayo inaungwa mkono wa hawamu ya nne ya Jamhuri ni ile ambayo, itawezesha kukabiliana kwa namna ya pekee katika kujaribu kutoa matatizo hayo ya nchi.

Katika waraka wao, maaskofu wamelezea juu ya wasiwasi wao mkubwa kuhusu uundaji wa hawamu ya nne ya Jamhuri ya nchi ya Chad. Mchakato huo kama wengi wanavyo ogopa unaweza kuleta hatari mbaya  ya sheria hasa   kuchezea demokrasia kwasababu ya kuzua au kuwa chanzo cha migawanyiko kati ya wazalendo wake. Kwa maana hiyo, Baraza la Maaskofu wa Chad wanakubaliana na suala hili kwa yule anayesema kwamba  hawamu ya nne ya Jamhuri ya Chad hajafanyiwa kura ya maoni ya wazalendo! 

Hata hivyo wanasema kwamba kati ya matukio ya sasa ya sera za  kisiasa, wanaona kuwa,  sehemu kubwa ya watu pia  wanadharau kile ambacho kinaendelea kutendeka, na kwa maana hiyo mabadiliko msingi ya asili, yanapaswa kufanyika na kuheshimu katiba yao ya Ibara ya 224 inayosema kwamba: mtazamo mpya wa Katiba unakubaliwa kwa kupitia kura ya  maoni!

Halikadahalika Maaskofu wa Chad hawakubaliani kabisa na matendo ya  Diya, yaani  juu hujuma ya uhalifu wa kumwaga damu  kwa njia ya sheria ya sharia. Na sababu yake ni kwamba inaondoa manai ya kijamii na nguvu zinazo unwa na haki za serikali, na pia kuongeza kuharibu uchumi katika jamii.

Kutokana na hiyo ni matumaini yao kwamba serikali inaweza kuongeza juhudi katika mfumo wa mahakama za serikali na kuondoa makubaliano ya jumuiya juu ya utumiaji wa Diya, kwasababu, imesababisha mivutano kati ya jumuiya mbalimbali. Mwisho waraka wa maaskofu unatoa ushauri kwa wahusika wote wa kisiasa, uchumi, jamii na dini katika nchi ili wote wafanye kazi kwa pamoja kwa ajili ya amani bila kusahau watu wake!

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.