2018-04-27 15:02:00

Juhudi ya Maaskofu wa Marekani katika sheria ili kuokoa DACA!


Mapendekezo yaliyotolewa na Maaskofu wa Marekani katika Bunge ili kuokoa mpango wa DACA yaani wa kutowarudisha  makwao  watoto wahamiaji, umepata msingi na sauti kubwa kwa mujibu wa maelezo ya Askofu Joe Vásquez, wa Tume ya wahamihaji ya Baraza la Maaskofu nchini Marekani. Waraka wao, uliowakilishwa katika Bunge la Marekani, unatazama michakato ya uraia karibia vijana laki nane, waliofika Marekani wakiwa wadogo na wazazi wao bila kuwa na vibali ruhusa halali, ambao kwa siku zilizopita kumekuwa ni mchakato wa hatari ya serikali ya Rais Trump kuwarudishwa katika nchi zao za asili, mara baada ya kusitisha mpango wa DACA,uliokuwa umewekwa kwa ajili ya ulinzi wao, wakati wa utalawa wa Rais B. Obama.

Katika Waraka mpya uliopewa jina la “Tuungane na kufanya Marekani kuwa na usalama” kuhusu Uraia lakini kuna  masuala mengine kama vile: hatua madhubuti ya kuthibiti wahamiaji haramu, shughuli za kiteknolojia ili kuhakikisha usalama wa mipaka ya Mexico; kuhusu kuongeza mahakimu  ambao watajikita katika suala la wahamiaji na mawakili wa tume ya wahamiaji; kutazama kwa makini maana ya kuweka utaratibu wa uwekezaji wa fedha kwa  nchi za Amerika ya Kusini kwa mtazamamo wa uthibiti wa wahamiaji katika siku sijazo na hata kuhusu masuala ya rushwa.

Maaskofu wa Marekani wanao utambuzi wa mapendekezo ya muda ambayo ni muhimu kwa kutoa suluhisho pana zaidi ili  kuunda mfumo wa wahamiaji ambao umekuwa na matatizo, lakini pia  wamechagua kutoa kipaumbele cha Dreamers na familia zao ambao kwa kipindi cha muda mfupi walikuwa hatari ya kutengena na watoto wao.

Askofu Vásquez, anathibitisha kwamba,ni matumaini  yao ya msaada wa sasa kwa mtazamo mpya wa sheria, unaweza kuendelea kuwa msaada wa DACA na kuwatia moyo Bunge la Marekani ili kujikita na kutenda kwa haraka kutafuta ufumbuzi wa sheria ya kibinadamu kwa ajili ya DACA na kukumbusha kuwa, wajibu wao kimaadili unajihusisha katika matendo ya dhati ya kulinda watoto hao.  Katika miezi hii maaskofu wa Marekani wamekuwa msaada mkubwa wa vijana wengi kwa kutambua mchango mkubwa ambao wameutoa katika nchi hiyo kwa mantiki ya kiuchumi, kitaaluma, kijeshi na shughuli mbalimbali katika maparokia zote nchini humo.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.