2018-04-27 15:57:00

Juhudi ya Caritas kitaifa na kijimbo nchini Uganda kwa ajili ya walemavu!


Wahudumu na wafanyakazi wa Caritas nchini Uganda  wako Kisubi kwasasa katika semina ya mafunzo juu ya maendeleo ya mtu kamili (DID) kwa lengo la kuhamasiha  ushirikishwaji kamili wa watu walemavu katika jamii (PWD).  Katika habari zilizotufikia kutoka Fides (shirika la habari za kimisionari, zinasema kuwa, zaidi washiriki 50 wakiwemo wafanyakazi wa Caritas ambao wanajumuisha mpango wa Caritas Jimbo, wahusika wa vyama mbalimbali kutoka katika majimbo 19 ya nchi, na wawakilishi wa serikali ya nchi, wapo wanajadiliana kuhusu mada ya Injili ya Mtakatifu Matayo “ Kisha akawambia nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo” (Mt2,8) ili kuweza kujikita katika matendo hai ndani ya jamii na Kanisa kwa ujumla.

Katika uthibitisho wa mkurugenzi wa utafiti na kisiasa wa Caritas nchini Uganda, Godfrey Oneth anasema kwamba, aina ya mafunzo yaliyopendekezwa kwa siku tatu za mkutano huo ni kutafuta namna ya kuweka katika mstari wa kwanza watu walio athirika katika mchakato mzima wa mpango wa Caritas wa kulinda na kutetea. Na mpango huo ni tofauti na mipango ya kiutamaduni ilizoeleka lakini ambayo hunapata nafasi kubwa ndani ya mipango ya Caritas kwa ngazi ya jimbo na hata kitaifa.

Aidha semina hiyo inataka kufanya utafiti mkubwa wa Tume ya Caritas nchini Uganda ili kuweza kuona mwanga wa ufunguo wa matatizo ya ulemavu na majibu ya sasa ambayo ni 8 kati ya 19 ya majimbo yote na zaidi ya kuweka ubora wa matendo na changamoto ndani ya majengo ya Caritas mahali ambapo sekta hiyo inafanya kazi.

Hata hivyo Maaskofu Shirikikisho la Baraza la Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA , wamethibitisha kuwa, washiriki wa semina hiyo wanapaswa kutazama kwa upya mipango ya sasa ya Caritas inayojikita katika masuala ya binadamu na zaidi kwa wale wenye ulemavu, ili kuweza kutambua jinsi gani ya kuweza kuwasadia zaidi hata wale ambao wamebaguliwa. Zaidi Wahudumu wa majimbo na wafanyakazi wa Caritas kitaifa  wanapaswa kufanya kazi kwa haraka katika mipango nyeti ya walemava kulingana na majimbo yao.

Shirika la Afya duniani inakadiria kuwa asilimia  10% ya watu duniani ni walemavu. Na kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za kitaifa nchini Uganda kwa mwaka 2002, watu 4 kati ya 25 ni walemavu katika  Bara la Afrika lenye kuwa  na wasiwasi mkubwa wa maendeleo. Watu walio na ulemavu kwa hakika wameonesha uzoefu hasi wa uchumi kijamii kulinganisha na wale wasio kuwa na ulemavu katika sekta ya ujenzi, afya ajira na zaidi kiasi kikubwa cha umaskini wa kukithiri. 

Kwa mujibu wa Ripoti ya takwimu ya idadi ya watu na juu ya sekta ya makazi mwaka 2014, ilikuwa asilimia 12,4 ambao walikuwa na umri usiozidi miaka 2, wakati katika rika la umri wa miaka 5 walikuwa ni asilimia 14%. Na ulemavu kwa ujumla nchini Uganda unahusu upofu, uziwi, viungo vya mwili, akili na hata ngozi (albino).

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.