2018-04-27 15:19:00

Hatimaye makanisa mapya 166 yapata kibali cha sheria kuanza huduma yake!


Kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume, Baraza la Mawaziri nchini  Misri wamekubali hivi karibuni kutoa kibali cha  sheria utambuzi wa makanisa 166 na majengo mengine ya Kanisa yaliyotawanyika katika maeneo ya nchi. Waziri Mkuu Bwana Sharif Ismil na waziri wa Ujenzi na huduma za jumuiya za vijiji, Bwana Mustafa  Madbouly wametoa uamuzi pia wa kutoa zana kila  iwezekanavyo za kuendeleza hatua za michakato ya sheria katika maeneo yote ya ibada ambayo bado hayajakubaliwa. Kwa njia hiyo viongozi wa Cairo wanathibitisha makubaliano ya uwepo wa madhehebu madogo ya kikristo, ambayo yalikuwa ni chanzo cha umwagaji damu kutokana na mashambuzi mengi yaliyotukia  kwa njia ya mikono ya makundi ya misimamo mikali ya kiislamu.

Kwa mujibu wa habari la gazeti la kila siku Misri ( Egypt today) , tume ambayo iliundwa mwezi Januari 2017, imepewa majukumu ya kutafiti vema na  kuhakikisha maombi yaliyotolea na jumuiya za kikristo ili kuachiwa huru au  kanuni ya Makanisa na maeneo yote nayoitazama  ibada, kwa mustakabali wa ibara ya 80 ya sheria ya nchi 2016, ambayo inaratibu ujenzi na ukarabati wa makanisa. Aidha kwa upande wa takwimu rasimi  za mnamo mwaka 2011, inaonesha kuwa nchini Misiri inayo makanisa 2, 869  na zaidi ya misikiti 108,000.

Makanisa ya Kiorthodox yametoa maombi ya makanisa 2,500 ya maparokia yao ambayo yanaridhisha na baadhi ya maeneo mengine ya ibada yanasadikika kujengwa zaidi ya miaka 150 iliyopita wakati  misri inatawaliwa na himata ya Ottomani. Andre Zaki mkuu wa Jumuiya ya kiinjili mahalia, amethibitisha kuwa, Kamati ya ndani imewakilisha makanisa 450 yakiwemo hata yale makanisa ambayo bado hayajaruhusiwa na kwa maana hiyo, ambayo bado hayajakubaliwa. Mengi ya hayo kwa hakika tayari yana nyaraka zinazoendana na ardhi ambayo ni matarajio ya ujenzi au kuhusu mchakato wa ujenzi ambao ulisitiishwa kwa muda na hata kusitishwa maadhimisho ya ibada zao. Habari hiyo inathibitisha  ukweli wa kukubaliwa  makanisa 166 yaliyoko katika maeneo ya wilaya na mikoa ya nchi ambapo wanategemea yaanze kutumika kwa miezi minne ijayo!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.