2018-04-26 17:04:00

Askofu Marcellin Kouadio Yao ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Daloa


Baba Mtakatifu Francisko amekubali na kuridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Maurice Konan Kouassi wa Jimbo Katoliki Daloa, nchini Pwani ya Pembe. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Marcellin Kouadio Yao kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Daloa, nchini Pwani ya Pembe. Itakumbukwa kwamba, Askofu Marcellin Kouadio Yao alizaliwa tarehe 10 Januari 1960 huko Vavoua.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 29 Desemba 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 1 Julai 2009 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Yamoussoukro, Pwani ya Pembe na kuwekwa wakfu hapo tarehe 22 Agosti 2009. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 25 Aprili 2018 amemteua kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Daloa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!

 
All the contents on this site are copyrighted ©.