2018-04-26 16:25:00

Askofu Alberto Arejula ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Nacala


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Germano Grachane wa Jimbo Katoliki la Nacala, Msumbiji. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu msaidizi Alberto Vera Arejula, OdM, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Nacala, nchini Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu Alberto Vera Arejula alizaliwa kunako tarehe 8 Aprili 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kipadre, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 14 Mei 1981. Baba Mtakatifu Francisko kunako tarehe 30 Machi 2015 akamteuwa kuwa ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Xai-Xai, Msumbiji na kuwekwa wakfu hapo tarehe 2 Mei 2015.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.