2018-04-25 14:21:00

Padre Bernardin Brou Daniel nchini Ivory Coast ameuwawa 23 Aprili 2018!


Habari kutoka Kanisa la Ivory Coast (Pwani ya Pembe) linaripoti kuwa padre,Bernardin Brou Aka Daniel, msaidizi wa Parokia ya Moyo Mtakatifu Koun-Abronso katika Jimbo Katoliki la Abengourou, Mashariki ya nchi ameuawa tarehe 23 Aprili 2018. Kwa mujibu wa habari zaidi kutoka Shirika katoliki la Fides, linathibitisha ya kuwa,jioni ya tarehe 23 Aprili Padre Bernardin alikuwa anarudi parokiani, akiwa katika barabara ya Agnibilekro- Koun-Fao  mara baada ya kuudhuria baadhi ya mikutano kadhaa huko jimboni Abengourou na ndani ya gari  alikuwa ameongozana na mmisionari mmoja, Padre Théophile Ahi majara ya saa 2:00 za usiku masaa mahalia.

Kabla ya kufika kwao kilometa chache  gari lao lililazimishwa kupunguza mwendo baada ya kuona lori moja likiwa limezuia njia. Katika harakati za Padre Bernardin kutafuta njia ya kukweka kizingiti, risasi ya moto zilimfikia kutoka kwa washambuiliaji wenye silaha waliojitokeza ghafula. Mara baada ya kujeruhiwa padre alilazimka kusimama na maharamia hao walitaka fedha lakini, mapadre hawakuwa nazo na hivyo bila huruma walimpiga risasi nyingine  ya tumbo. Na wakati wanaendelea na ukatili huo, gari moja lilitokeza, ambalo liliwafanya maharamia hao kutokomea na kumwacha Padre Bernardin lakini akipoteza damu nyingi ambapo hata mara baada ya kufikishwa hospitali mahalia, alikata roho kutokana na majeraha makubwa aliyopata!

Padre Bernardin Brou Aka Daniel alizaliwa Desemba 1976 na kupata daraja Takatifu la Upadre mnamo 2013. Ametoa huduma yake ya kichungaji katika  Parokia ya Appouessou  ya Mkatakatifu Joseph  wa Amelékia; katika Parokia ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu huko Apprompronou kabla ya kuhamishwa katika Parokia Koun-Abronso ya  Moyo Mtakatifu mahali ambapo alikuwa akitoa huduma yake ya kichungaji. Raha Milelele ampe ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie, apumzike kwa amani Amina!

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.