2018-04-25 14:58:00

Milioni 216 ya visa duniani na vifo 445,000 kwa mwaka kutokana na Malaria!


Malaria bado ni sababu ya kwanza inayosababisha vifo vya watoto wadogo na magonjwa katika nchi 91 za kitropiki katika  vifo 445,000 kwa mwaka. Na moja ya mkakati mkubwa wa mapambano ya malaria ni kuthibiti mbu wa Anopheles anayeambukiza kwa njia ya viruwi ruwi vya malaria kwa binadamu. Kwa mara ya kwanza katika muongo mmoja uliopita hatua za kuelekea kutokomeza malaria zimekwaa kisiki na mafanikio yaliyo patikana kushuhudiwa kubadili mwelekeo katika baadhi ya nchi zote duniani. Hayo yamesemwa na shirika la afya ulimwenguni WHO tarehe 25 Aprili wakati wa kuadhimishwa siku ya malaria duniani, na kuongeza kuwa, mwaka 2016 umekuwa na visa milioni 216 huku vifo 445,000 vikiripotiwa kutokana na ugonjwa huo hatari. 

Akizungumza mjini Geneva Uswisi Pedro Alonso, mkurugenzi wa mpango wa kimataifa wa malaria amesema, kauli mbiu ya siku ya malaria mwaka huu ni “Tayari kuitokomeza malaria” kwani kwa sasa dunia imefikia ukomo wa kuona ni nini inaweza kufanikiwa kwa rasilimali chache zilizopo na hivyo  amesisitiza kuwa, mafanikio ya vita dhidi ya malaria yanahitaji kufufua utashi wa kisiasa, kuongeza rasilimali fedha kutoka kwa nchi wahisani na nchi zilizoathirika na malaria na pia nyenzo mpya na zilizoboreshwa za kupima na kutibu malaria.

Lengo kuu likiwa kuzisaidia nchi zinazobeba mzigo mkubwa wa ugonjwa la malaria ambazo nyingi ziko Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, kanda ya Afrika bara linalobeba asilimia 90 ya mzigo wa malaria na asilimia 91 ya vifo vyote vya gonjwa hilo. Hayo ni kwa mujibu wa Daktari, Matshidiso Moeti mkurugenzi wa WHO ambapo naongeza na kusema kuwa  wao kama ukanda wa Afrika, viongozi wao  wa kitaifa na serikali zao lazima zichukue hatua za makusudi kuongeza uwekezaji katika sekta ya afya lakini pia watambue kuwa kinga dhidi ya Malaria  na tiba ni uwekezaji mzuri.

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO imetoa wito wa hatua za haraka kurejesha vita vya kimataifa dhidi ya malaria katika msitari unaotakiwa baada ya kwenda kombo, ili kufikia lengo namba 3.3 la Maendeleo endelevu (SDGs) la kuutokomeza ugonjwa huo ifikapo 2030. Watoto chini ya umri wa miaka 5 kwa namna ya pekee wanashambauliwa sana na kuongezeka kwa magonjwa makubwa.

Na zaidi ya asilimia 70 ya waliugua ni kutokana na malaria, ambao karibu kwa miaka hiyo asilimia 80% ni kutoka nchi za Afrika chini ya jangwa la sahara. Katika kanda hizo asiliomia 19% ya watoto walioshambuliwa na malaria wanaoweza kupata matibabu ya mwanzo kwa dawa iitwayo artemisina, lakini kila dk 2 wanakufa kwa ugonjwa wa malaria. Suluhisho la mkakati wa kuthibiti malaria unahitaji dhamiri ya kina ya kibaiolojia hasa katika aina ya mbu ambao wako katika nchi za Afrika  Kusini chini ya jangwa la sahara!

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.