2018-04-24 15:13:00

Siku ya Malaria Duniania:Inawezekana hata kwa njia ya mafunzo!


Nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inaendelea kuishi katika hali siyo kuwa na msimamo, kutokana na kwamba  sehemu kubwa ya vifo vimesababishwa na vurugu ambazo bado zinaendelea hata sasa  zaidi ya lishe na matokeo yake. Kwa mfano malaria na ukosefu wa vyakula pia umesababisha majanga makubwa na zaidi kwa upande wa watoto. Utapia mlo wa kukithiri umedhoofisha kinga za mwili na hivyo kuwa rahisi kukumbwa na magonjwa ya mlipuko zaidi hata  kwa upande wa magonjwa ya Malaria.

Katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya kupambana na  Malaria inayo adhimishwa kila ifikapo tarehe 25 Aprili yak ila mwaka, mwanafunzi wa Chuo cha Kisayansi cha uuguzi (ISSI) kilichopo Kishasa (DRC), lakini kwa msaada wa wafadhili  yupo mazoezi yake katika Chuo Kikuu cha Wauguzi Roma ametoa ushuhuda wake katika Gazeti la Fides.
Yeye ansema kuwa, sehemu ya Mont-Ngafula mahali kilipo chuo cha Wauguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndilo eneo hasa lenye kipeo cha vurugu kwa sasa, lakini wao wako tayari kutoa huduma kwa kila sehemu ya nchi, mahali ambapo kuna ulazima. Muunguzi anayepata mafunzo kutoka katika chuo hicho kwa haraka anapata kazi kwasababu ya maandalizi ya taaluma na kibinadamu inakwenda sambamba.

Aidha amesema kuwa, mfumo wa afya kwa hakika hautoi  zana muhimu kama vile madawa na zaidi mafunzo ya watu muhimu ya kuweza kusaidia ubora wa matibabu,hivyo wagonjwa wengine hawezezi kupata matibabu yanayo stahili. Kwa mfano malaria, zipo dawa zinazofaa, kama mgonjwa akitibiwa na dawa inayostahili, lakini gharama ni kubwa kumwezesha mgonjwa wa kawadia kupata tiba inaystahili. Kutokana na suala gharama za madawa, wao kama wauguzi wanashauri juu ya elimu na hivyo kufundisha njia ya kuzuia, kwa sababu ya utambuzi ya kwamba mtu ndiyo kitovu.

Hata hivyo pamoja na ushuhuda wa mwanafunzo huyo habari nyingine inasema kuwa; Madaktari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea na mgomo wao walioanza siku ya Jumatatu kwa wito wa chama chao kikuu. Madaktari nchini (DRC) Congo wanaomba serikali kuboresha mishahara yao, huku wakiishutumu kutoheshimu makubaliano walioafikiana mwaka jana kuhusu madai yao.

Madaktari wanadai kupewa mshahara mzuri, malipo ya kazi zao za ziada, kutambuliwa kwa vyeo vyao na ufumbuzi kwa madaktari mia moja waliyofukuzwa kinyume cha sheria mwaka 2016 kwa mujibu wa madaktari hao, na ambao hufanya kazi tangu wakati huo bila malipo.
Jambo muhimu zaidi, madaktari wanalalamikia makubaliano ya hivi karibuni yaliyosainiwa mnamo Septemba 2017 na yangelipaswa kutatua masuala yote hayo yanayozua utata. Kwa mujibu wa madaktari makubaliano hayo hayajawahi kutekelezwa.

Hata hivyo wagonjwa wameomba madaktari kusitisha mgomo huo wakisema kuwa unawaathiri sehemu kubwa, huku wakiomba serikali kutafutia ufumbuzi madai ya madaktari. Hata hivyo mwishoni mwa wiki iliyopita, serikali ilitoa mapendekezo kwa madaktari wanaogoma. Serikali inabaini kwamba tayari imejibu madai ya madaktari, huku ikisema kazi kubwa kwa sasa iko upande wa chama kikuu cha madaktari, ambacho hakikuwasilisha mapendekzo hayo kwa wanachama wake. Kwa wakati huu, hakuna mkataba umefikia.

Sr Amgela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.