2018-04-22 15:18:00

Jumapili ya Kristo Mchungaji mwema ni Siku ya kuombea Miito Dunaini


Mara baada ya sala ya Malkia wa mbingu, Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 22 Aprili 2018 ameonesha wasi wasi mkubwa kwa kile ambacho kinaendelea kutukia nchini Nikaragua, baada ya maandamano makubwa ya kijamii  kusababisha  machafuko makubwa ambayo pia yamesababisha waathirika na majeruhi wengi. Kwa njia hiyo anaonesha ukaribu wake katika sala kwa nchi hiyo pendevu na kuungana na maaskofu, ili kuomba kusitishwa kwa kila aina ya vurugu na nguvu, ili kuweza kuzuia kuendeleza umwagaji damu, na masuala yaliyofunguliwa yaweze kupata suluhisho  kwa amani na maana ya uwajibikaji.

Halikadhalika amekumbusha, kama alivyomaliza kuelezea kuwa Domenika ya nne ya Pasaka katika  Kanisa zima linaadhimisha Siku ya Maombi ya miito duniani. Siku inayoongozwa na mada ya “kusikiliza, kung’amua na kuishi wito wa Bwana”. Anashukuru Mungu kwasababu ya kuendelea kutoa historia ya upendo katika Kanisa ,kwa ajili ya Yesu Kristo, sifa na utufuku wake kwa hudumia  ndugu. Leo hii kwa namna ya pekee anawashukuru mapadre wapya alio wapatia Daraja Takatifu la Upadre katika Kanisa la Mtakatifu Petro. Kwa maana hiyo anaomba kwa Bwana aweze kutoa wafanyakazi wengi na wema katika  shamba lake,hata kuongeza miito ya maisha ya kitawa na ndoa ya kikristo. Amewasalimia mahujaji na waamini kutoka pande za dunia na kuwatakia matashi mema ya Siku ya Jumapili, bila kusahau kuomba sala kwa ajili yake! 

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.