2018-04-21 15:30:00

Upendo wa Mungu na Jirani ni ushauri wa Papa kwa Waseminari wa Uingereza!


Ninawakaribisheni wakuu na wanafunzi wa Taasisi ya Kingereza , ambayo mwaka huu inakumbuka kwa namna ya pekee ya miaka ya maisha ya Kanisa la Uingereza na Galles. Namshukuru Gombera kwa maneno ya hotuba yake.  Na mkutano wangu leo hii unanipa fursa ya kuongea nanyi moja kwa moja kama baba kutoka moyoni! Wakati mnaendelea katika hatua za mchakato wa safari ya kujibu wito wa Bwana, ninataka kushirikishana nanyi baadhi ya maneno ya kuwatia moyo. Zadi ninawaombea ili ninyi mpate kukua kwa kutafakari kwa kina daima kuhusu uhusiano wenu na umakini kwa wengine na zaidi wale ambao waahitaji. Tafakari hii ni juu ya  Upendo wa Mungu na upendo wa jirani; ndiyo mawe mawili yenye thamani ya maishia yenu.(Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.  Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi (taz Mk 12,30-31).

Ni utangulizi wa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko,alipokutana na wakuu na wanafuzni wa Taasisi ya Uingereza iliyo mjini Roma Jumamosi 21 Aprili 2018 mjini Vatican. Baba Mtakatifu akianza ufufanuzi wake juu ya maneno ya kuwatia moyo amesema: la kwanza ni upendo wa Mungu. Ni vizuri kutazama vijana wanajiandaa kushika wajibu wa kuwa na msimamo na Bwana ambao unadumu maisha yote. Lakini hiyo ni ngumu kwao kama jinsi ilivyokuwa ngumu hata kwa upande wake, haza zaidi kutokana na maisha ya sasa ya utamaduni wa mpito. Ili kushinda changamoto hii na ili kuweza kuwasaidia katika udhati wa ahadi kwa Mungu, ni lazima kumwilishwa maisha ndani wakati wa mchakato wa maisha yao  ya kuwa seminarini, wakijifunza namna ya kufunga milango yao ya nyumba ya undani. Kwa namna hiyo huduma ya Mungu na Kanisa itaonesha nguvu na kupata ile amani na furaha ambayo ni Yesu peke yake anaweza kuitoa. (“Ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.) ( taz Yh  14,27). Kwa njia hiyo kama mashuhuda wa Kristo kwa mara nyingine, wanaweza kumshangilia na kuwa kama Mtakatifu Filipo Neri, na kama babu zao mashahidi: “Salvete flores martyrum!”.

Neno la pili la kuwatia moyo, Baba Mtakatifu anasema ni upendo wa jirani: Akifafanua namna gani anasema: kama wanavyotambua kuwa mashuhuda wa Kristo si kwa ajili ya  manufaa yao binafsi, bali ni kwa ajili ya wengine katika huduma ya dhati. Wao wanachojaribu kutenda ni kutoa huduma hiyo si kwa ajili ya hisia rahisi, badala yake ni utii kwa Bwana ambaye aliinanama na kupiga magoti kuwanawisha mitume wake (taz Yh 13,34).  Kwa maana hiyo hata kumfuasa  katika njia yao ya kimisionari haiwezi kuishia  tu kiupweke, kinyume chake ni kushirikishana na wengine mapadre, watawa, walei waume na wake. Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba, wakati mwingine ni vigumu kupenda jirani, na ndiyo maana  ya shughuli yao ya kichungaji, ili iweze kuwa ya dhati na  inatakiwa daima ibaki kidete na Mungu ambaye anapenda na kusaidia. ( Wosia wa Gaudete et Exsultate, 112). Uthibitisho huo wa kina, imani ya upendo, ilikuwa ni mtindo wa maisha ya wafia dini wa Taasisi yao na ni muhimu kwa wote wanaotafuta na  kumfuata Yesu anaye waita katika umaskini wao ili kumtumikia ukuu wake na anaye jionesha ukuu huo kati ya maskini.

Vilivile anasema kwamba moja ya aina za kuweza kukua katika upendo kwa Mungu na jirani ni kwa njia ya maisha ya jumuiya. Na hiyo inajionesha wazi ya iliweza kutendeka uzoefu huo kwa mana siyo rahisi kuona kwamba Jumuiya yao katika Seminari hiyo waliweza kutoa wafiadini 44, na kuona kwamba unakuwapo  uwezo wa kuwa tayari kutoa kiapo cha umisionari kwa mara ya kwanza mwaka 1578 na Mtakatifu Ralph Sherwin siku ya  sikukuu ya Mtakatifu George!  Kwa maana hiyo baba Mtakatifu anahimia kwamba kwa njia ya maongozi hayo na kuiga watakatifu hao, ni matumaini ya yake  watakuwa na uwezo wa kuendeleza ule undugu wa utakatifu, wa kutafakari na kutambua, kutazama ukuu wa utakatifu wa jirani, mahali ambapo unagundua Mungu kwa kila binadamu, na kutambua uvumilivu kwa yote ili kuweza kuishi kwa pamoja. (Wosia. Evangelii gaudium, 92

Katika maisha ya kikristo kuna kizingiti kukubwa mbele ya kila mmoja, ambao ni woga. Baba Mtakatifu anasema, lakini kwa upande wao wanaweza kuushinda kwa njia ya upendo na kuwa wakarimu (taz Wossia Gaudete et exsultate, 126) kwanjia ya  sala aliyo andika Mtakatifu Thomas Moro ). Kwa namna hiyo ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, hawatakuwa na hofu ya matatizo, majaribu na mapambano ya kila siku dhidi ya dhambi. Vilivile anawatia moyo zaidi wasiwe na hofu binafsi. Kwa kufuata mfano wa Msimamizi wao Mtakatifu Thomas wa Canterbury, ambaye hakuruhusu dhambi za wakati ulio pita ziwe kizingizi cha binadamu au kumzuia kuhudumia Mungu hadi mwisho; zaidi hawataweza kushindwa vizingiti  vya hofu badala yake watawasaidia wengine kishinda.

Na mwisho amehitimsha kwa kuwaomba waimarishe urafiki, mwema na mahusiano yaliyo mema katika huduma yao ijayo na kwa hakika waweze kutambua marafiki wa kweli ambao si tu wale wanaonekana na mamoja kati yao, bali kuwaona kama zawadi ya Bwana ili kuwasaidia katika hija yao kuelekea kile kilicho na sifa njema na haki. (“Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.) (taz Fil 4,8).

Kwa upendo Baba Mtakatifu amewaachia mawazo hayo ili kuwatia moyo katika upendo mwaminifu wa Mungu na katika huduma ya unyenyekevu kwa ndugu kaka na dada. Amewakabidhi kwa maombezi ya Mama Maria wa Walsingham na kuwahakikishia maombi yake kwa ajili ya familia zao na wale wote wanaosaidia Taasisi hiyo yao ya Uingerza mjini Roma. Kwa mara nyingine tena anawaomba wasali kwa ajili yake.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.