2018-04-20 17:24:00

Papa:Mfano wa Don Tonino wote tunaweza kuwa kisima cha matumaini!


Katika masomo mawili yaliyosomwa yanawakilisha mambo msingi mawili ya maisha ya kikristo, yaani mkate na Neno. Mkate ni chakula muhimu kwa ajili ya kuishi, na Yesu katika Injili anajiita kwetu kama mkate na maisha kwa njia ya kueleza kuwa bila yeye hatuwezi kufanya lolote. Ni utangulizi wa mahaubiri ya Baba Mtakatifu Ijumaa, tarehe 20 Aprili 2018 wakati wa maadhimishi ya misa takatifu kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 25 tangu kifo cha Mtumishi wa Mungu Dono Tonino Bello aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Molfetta nchini Italia. Alikufa kwa ugonjwa wa saratani lakini akiwa na maisha ya utakatifu.

Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake anasema neno lilisikika la Yesu ni  tamko la nguvu zaid lisemalo “kuleni mwili na kunya damu yangu (taz Yh  6,53) .Je ni nini maaa yake ? Katika maisha yetu ni muhimu kuingia katika uhusiano wa maisha binafsi na Yey.  Mwili na Damu, yaani Ekaristi siyo kusema ni ibada nzuri tu, badala yake ni muungano wa kina ambao daima unashangaza kwa maana ya fursa ya kuweza kujifananisha na Mungu: muungano wa upendo wa dhati ambao unajitokeza wakati wa kula makate huo. Kila maisha ya mkristo yanaanzia hapo, katika karamu mahali ambapo Mungu anatushibisha upendo wake. Bila Yeye, yani bima Mkate wa maisha kila aina ya juhudi katika Kanisa ni bure, kama anavyokumbusha Askofu Tonino Bello ya kuwa: “haitoshi kufanya ya upendo tu iwapo huna upendo katika matendo”. Iwapo unakosa kianzio, yaani mahali ambapo Ekaristi inaanzia, kila aina ya shughuli ya kichungaji ni bure, Baba Mtakatifu anathibitisha.

Yesu katika Injili inathibitisha: “kila alaye Mwili wangu ataishi kwa ajili yangu”. Hiyo ina maana ya kusema kila anayeshibishwa Ekaristi anafanana na mawazo Bwana. Yeye ni mkate uliomegeka kwa ajili yetu na kila aulaye anageuka, kuwa  mkate uliomegeka, ambao haujatiwa chachu  ya kiburi, lakini mkate unaojitoa kwa wengine: hajifikirii binafsi na mafaniko yake tu, badala yake  ni kwa ajili ya wengine hasa baada ya Misa.

Baba Mtakatifu anatoa mfano kwamba Ni kuiishi kwa ajili ya wengine anayekula mkate huo kwa maana ni chapa ya kiwanda cha kikristo na inawezakana hata kuweka maandishi hayo nje ya kila Kanisa “Baada ya Misa siyo kuishi binafsi baadala yake ni kuishi kwa ajili ya wengine”
Baba Mtakatifu Francisko anaendelea na tafakari kwamba Askofu Tonino aliishi hivyo kati yao ambaye ni mtumishi wa Mungu, na ambaye kwa hakika alikuwa mchungaji wa matendo wa watu wake, na ambaye mbele ya Tabernakulo alijifunza kushibishwa na watu wake. Alikuwa kiota Kanisa lenye kiu ya Yesu kwasababu ya kupenda kushikilia kila aina ya malimwengu; alikuwa anaota  Kanisa ambalo linatambua mwili wa Kristo katika Tabernakulo za majanga, mateso na upweke. Yeye alikuwa anasema “Ekaristi haikubaliani na uvivu bila kuamka mezani na kubaki sakramenti isiyokamilika”.

Kutokana na hili, twaweza kujiuliza, je Sakramenti inajikamilisha namna gani kwa dhati katika maisha yangu?, Je ninapendelea kuhudumiwa tu meza ya Bwana au ninaamka kuwahudumia kama Bwana? Na kama Kanisa tunaweza pia kujiuliza, baada ya kupokea kumunio nyingi je tumekuwa watu wa muungano?   Mkate wa maisha, uliomegeka kwa ajili yetu pia ni mkate wa amani. Askofu Tonino alikuwa anasema: “haiwezekani kupatikana amani iwapo mtu ananunua mkate na kula peke yake…..Amani ni jambo kuu zaidi ha hilo, ni kuishi kwa pamoja: Ni kula mkate pamoja na wengine bila kutengena au kutenganisha meza kati ya watu wengine tofauti, mahali ambapo kuna mwingine ndipo unagundua  uso na kutafakari pia  kubembeleza. Kwasababu migogoro na vita vyote vinapata mizizi kutokana na ukosefu wa usawa na utengeno.  Sisi tunaoshiriki Mkate huo wa umoja na amani, tunaalikwa kupenda kila aina ya uso na kushona viraka vilipopasuka;halikadhalika  kuwa wajenzi wa amani kila mahali daima!

Baba Mtakatifu akichambua neno sehemu ya pili   kuhusu Neno anasema:Katika Injili imesikika watu waliomzunguka Yesu wakinungunika kuwa “inawezekanaje huyo kutupatia mwili wake na kula”. Kulikuwa na hali ya kushangaza katika maneno hayo, Baba Mtakatifu anathibitisha na kuongeza kuwa: mara nyingi maneno hayo yanafanana na yetu katika nyakati hizi ya kusema:jinsi gani Injili inaweza kutoa la matatizo ya dunia? Je  inanisaidia nini kutenda wema katikati ya mabaya? Na kwa njia hiyo hata sisi tunaangukia katika makosa yaleyaleya  watu ambao walikuwa wamelemaa na kujadili   maneno ya Yesu, badala ya kupokea na kuyaishi katika maisha jinsi alivyokuwa akiwaalika.

Walikuwa hawatambui ya kuwa Neno la Yesu ni kwa ajili ya kutembea katika maisha ya kweli na siyo katika kukaa na kuzungumza kile ambacho kinakwenda au kisichokwenda. Askofu Tonino wakati wa kipindi cha Pasaka alikuwa akiwalika watu wake, kupokea habari mpya ya maisha,hili hatimaye maneno hayo yaweze kujikita katika matendo ya dhati. Kwa maana hiyo alikuwa akiwashauri hasa ambao hawakuwa na ujasiri wa kubadili maisha yao, wataalamu wa mshangao; Wahasibu na wapiga hesabu wanaotaka kupata faida bila kuhangaika.

Yesu hakujibu kwa mantiki za hesabu yao,yaani za kuishi kwa wakati tu, badala yake alijibu ndiyo ya daima yaani kwa maisha yote. Kwa maana yeye hakutafuta tafakari namna yetu bali uongofu wetu.Baba Mtakatifu amehitimisha  mahubiri yake kwamba kila Misa tunalishwa Mkate wa maisha na Neno ambalo linatoa wokovu. Tunaishi kile tunacho adhimisha na kama Askofu Tonino, wote tunaweza kuwa kisima cha matumaini, cha furaha na  amani!

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News!








All the contents on this site are copyrighted ©.