2018-04-20 16:00:00

Papa:Don Tonino Bello alikuwa kama Kanisa linalowaka upendo!


Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake, amemtafakari Askofu Tonino Bello wametazama mambo makuu matatu kwamba, alikuwa kama Kanisa linalowaka upendo, hakujalia ukuu na hata sifa, na alikuwa amesimika miguu ardhini lakini macho yake yakiwa yanazama juu angani. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu wakati wa hotuba yake ameanza akisema: nimefika kama mhujaji katika ardhi hii iliyo mpatia maisha Mtumishi wa Mungu Tonino Bello. Nimemaliza kusali mbele ya kaburi lake ambalo siyo kito cha nakishi kilichosimama juu bali kilichopandwa ardhini: Don Tonino aliyepandwa katika ardhi yake ni kama anataka kutueleza jinsi gani alipenda eneo lake. Baba Mtakatifu ametafakari hawali ya yote kupitia maneno yake ya shukrani. “Asante ardhi yangu, ndogo na maskini ambayo imenizaa maskini kama wewe lakini kwayo imenipa utajiri usi ona kifani, kutambua umaskini na kuweza kijikita leo hii kuwatumikia”.

Kuwatambua maskini ndiyo ulikuwa utajiri wake, baba Mtakatifu anathibitisha. Alikuwa na sababu kwani maskini kwa dhati ndiyo utajiri wa Kanisa. Ni kukumbusha jinsi gani Don Tonino alikuwa anaishi mbele ya vishawishi vinavyokwenda nyuma ya wenye nguvu, wanaotafuta faida na furaha na wanaotaka kuishi maisha mazuri. Kwa njia ya Injili kwa kawaida alikuwa ikiwakumbusha Noeli na Pasaka ambayo inawaalika katika maisha yale ambayo hayastahili ili waweze kutafuta Yesu anayependa maskini walio wanyenyekevu. Ndivyo alivyofanya Mwalimu,  ndiyo alikuwa na Mama yake akimsifu Mungu kwasababu amewashusha wenye nguvu kwenye viti vya na kuwakweza wenye upole. (Lk 1,52). 

Kanisa ambalo linajikita kwa moyo wote kwa ajili ya maskini linabaki daima kama mfereji wa Mungu, haupotezi daima mwendelezo wa Injili bali kuwa daima na  ulazima wa kurudi katika mambo yaliyo ya msingi na kusadiki kwa dhati Bwana aliyw mwema peke yake.

Baba Mtakatifu anasema, Don Tonino anatualika kutofanya nadharia mbele ya maskini, badala yake ni kuwakaribia kama alivyofanya Yesu kwetu sisi, yaani jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. (taz 2 kor 8,9). Don Tonino alihisi mahitaji ya kuiga  na kujikita akiwa mstari mbele.  Hakusumbuliwa na maombi mengi  hata waliotaka kumchukiza. Hakuogopa ukosefu wa fedha badala yake aliahangaikia wenye ukosefu wa ajira, matatizo ambayo hata leo hii bado yanaendelea. Hakukosa fursa ya kuwa mstari wa mbele hasa katika kutetea hadhi ya  wafanyakazi na kila kiumbe walio wadhaifu

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News! 
All the contents on this site are copyrighted ©.