2018-04-19 16:32:00

Papa anasema:karama ya wabenediktini ni sala,kazi na mafunzo na kupokea!


Katika fursa ya kuadhimisha Jubilei ya miaka 125 ya Shirikisho  la Wamonaki wa  Mtakatifu Benedikto, wamekutana na Baba Takatifu Francisko mjini Vatican, tarehe 19 Aprili 2018. Wakati wa kutoa hotuba yake, ameshukuru Abate kwa maneno yake na kuwashukuru kwa mchango wao, wanao utoa kwa maisha ya Kanisa, kila pande ya dunia na kwa  karibu ya  miaka miatano hivi. Katika jubileo yao ya  Shirikisho la watwa wa kike wa Mtakatifu Benedikto,  Baba Mtakatifu anasema, wanataka wakumbuke kwa namna ya pekee Papa Leone wa XII ambaye mnamo mwaka 1893 alipendelea kuunganisha watawa wa kike wa Shirika la Mtakatifu Benedikto  kwa kuunda nyumba ya pamoja ya mafunzo na sala, mjini Roma. Ni jambo la  kumshukuru Mungu  hasa kwa kumpata maongozi hayo kwa dunia nzima na zaidi ile roho ya upamoja na kiti cha Petro, kati yao.

Tasaufi ya wabenediktini  inajulikana kwa nembo ya “Ora et Labora et Lege” yaani sala, kazi na mafundisho. Katika maisha ya kutafakari Mungu mwenyewe anatangaza uwepo wake kwa namna isiyotarajiwa. Kwa tafakari ya Neno la Mungu na masifu ya Mungu, tunaalikwa kubaki ndani ya dini katika kusikiliza sauti yake ili kuweza kuishi kila siku na furaha ya utii. Maombi yanazaa ndani ya mioyo yetu kuwa tayari kupokea zawadi za kushangaza ambazo Mungu daima yuko tayari kutoa, upyaisho wa roho inasaidia kujikita katika kazi zetu za kila siku, kutafuta namna ya kushirikishana zawadi ya hekima ya Mungu na wengine: kwa jumuiyua na wengine wanaokuja katika monasteri  ili kumtafuta Mungu (“quaerere Deum”), na wengine ambao wanajifunza katika shule zao, yaani taasisi  na vyuo vikuu. Kwa maana hiyo tasaufi  inazaa daima upyaisho na ujana wa maisha ya kiroho.

Iwapo Mtakatifu Benedikto alikuwa ni nyota angavu kama alivyokuwa akimwita Mtakatifu Gregori Mkuu, katika enzi zake, kwa maana  kulikuwa na kipeo cha kina cha thamani na mapokeo, kwa maana hiyo alitambua namna ya kung’amua kati ya mambo msingi na katika maisha ya kiroho ili kuweka msimamo katika kitovu cha Bwana. Kwa maana hiyo, watawa hawa wanaweza kuwa kama watoto wa nyakati hizo ili kujikita katika matendo ya dhati ya kung’amua na kutambua kile kitokacho na Roho Mtakatifu na ambacho kinatoka katika roho ya dunia au roho ya shetani. Ni mang’amu ambayo si katika kutoa utashi na uwezo wa kuwa na sababu au maana ya upamoja tu, badala yake Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, ni zawadi ambayo lazima kuiomba kwa roho Mtakatifu. Bila hekima ya mang’amzi tunaweza kugeuka kwa urahisi vinyago vya kibiashara kama tabia za wakati  huu» (taz Gaudete et exsultate, 166-167) .

Katika enzi hizi mahali ambapo watu wanajihusiha sana na shughuli zao, hadi kukosa muda wa kutosha kusikiliza sauti ya Mungu, monasteri z o na koventi zao zinaeuka kuwa kama chemichemi, mahali ambapo waamini wa kila rika, rangi, utamadini na dini wanaweza kuja kugundua ule uzuri wa ukimya na kujitafuta wao wenyewe nafis zao katika hali ya upendo wa uumbaji, kusikia msimamo wa Mungu ambao ni radha ya maisha yao ya kila siku. Karama ya wabenediktini katika kukaribisha ni tunu msingi wa uinjilishaji mpya, kwasababu inatoa fursa ya kumpokea Kristo kwa kila nafsi kwa yule anayekuja na kumsaidia yule anayetafuta Mungu apate zawadi za kiroho ambazo yeye mwenyewe anaweka kwa kila mmoja wetu.

Wabenediktini daima wanajulikana katika shughuli ya kiekumene na mazungzmo ya kidini, kwa maana hiyo anawatia moyo ili waendelee katika shughuli hii muhimu kwa ajili ya Kanisa na dunia, kujikita katika huduma hiyo haya ya utamaduni wa makaribisho. Kwa dhati hakuna tofauti kati ya maisha ya sala na huduma kwa wengine, Monasteri za kibenedektini katika miji, hata mbali na miji zimekuwa daima maeneo ya sala na makaribisho. Msimamo wao ni muhimu hata kwa watu ambao wanakwenda kuwatafuta. Kristo yupo katika makutano hayo kwa mmonaki, muhaji na mwenye kuhitaji.

Baba Mtakatifu amerudia kuwaeleza juu ya utambuzi wa huduma ya kambi zao za elimu na mafunzo mjini  Roma na sehemu mbalimbali za dunia. Wabenedikiti wanajulikana kwa huduma ya Bwana na wameweza kutoa wanafunzi wengi kwa pamoja ambao ni muhimu katika utambuzi na zana ambazo zinaweza kukusanya ile hekima ambayo inasukuma kutafuta daima Mungu katika maisha: hekima ile ambayo itawafanya waendelee kujikita katika utambuzi wa pamoja  kwababu sisi tu wana wa Mungu kaka na dada katika dunia ambayo inayo kiu na amani. Mwisho anawatakiwa maadhimisho mema ya jubilei yao tangu kuanzishwa kwa Shirikisho la watawa wa kike wa Mtakatifu Benedikto  na ili waweze kutafakari kwa kina juu ya kutafuta Mungu na hekima yake ikiwa  pia   kuonesha kwa dhati utajiri wake kwa kizazi endelevu. Kwa maombezi ya Bikira Maria Mama wa Kanisa na Muungano wa Kanisa hai na watakatifu Benedikto  na Skolastika amewapatia baraka ya kitume na kuomba wasali kwa ajili yake pia.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.