2018-04-18 16:20:00

Semina kuhusu Bikira Maria kwa Mabalozi wa Vatican!


Jumatatu 16 Aprili 2018 imefanyika semina kuhusu Taalimungu  ya Bikira Maria kwa mabalozi wote wa Vatican. Ni tukio linalotaka  kufungua mchakato kati ya Taasisi ya Taalimungu ya Bikira  Maria na viongozi wa kidiplomasia ili kwa pamoja kuweza kutafuta njia za maendeleo zaidi katika upendo na amani. Semina hiyo imefanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha  Antonianumu Roma cha ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Assisi, mahali ambapo pia kuna Taasisi ya  Kipapa ya Taalimunguya Bikira Maria Kimataifa, taasisi ya kipapa iliyoanzishwa na wawafranciskani wenyewe , ikiwa  kama pete inayounganisha kati ya wasanii wa Taalimungu ya  Bikira Maria kwa Wakristo wote!

Taasisi hiyo ilianzishwa tangu Julai 1946 na ndugu wadogo wafransiskani mwanzo wakiwa wanatoa vitabu juu ya Maria katika maktaba yao; wao pia  walikuwa na wajibu wa kuandaa masomo yanayohusu mafundisho sadikifu ya Kanisa kuhusu Bikira Maria mkingiwa wa dhambi ya asili,  wakati wa kuandaa maadhimisha ya miaka 100 tangu kutangzwa kwake.  Mnamo tarehe 8 Desemba 1959 Papa Yohane wa XXIII kwa barua yake binafsi (the motu proprio Maiora), kabla ya kifo chake alitoa jina la Taasisi hiyo ya Kipapa. Kwa maana hiyo taasisi imeundwa na kamati ya kudumu ikiwa inaandaa maadhimisho ya Kimataifa  na mikutano ya Taalimungu na Kongmano kuhusu Bikira Maria. Kamati hiyo ilikubaliwa na Mtakatifu Yohane Paulo  II kuwa sehemu rasimu ya Taasisi hiyo. Katika semina ya wanadiplomasia wa Vatican, imeongozwa na Padre Stefano Cecchin Mwenyekiti wa taasisi hiyo ( Pontifical Academy of Mary Internationalis), PAMI. Mara baada ya semina hiyo mwandishi wa habari ameonana na Padre Checchin ili apate kuelezea lengo zaidi la kufanya semina hiyo kwa wanadiplomasia wa Vatican.

Padre Chechin anasema, wanadiplomasia wanayo shughuli nyeti, ya hali ya juu kwa kuwa wao ni  kama mawakili katika sera za kisiasa. Na wao kama wanashirika la kifransiskani,wanayo wajibu wa kutaka kurudisha sura ya mwanamke katika hali yake ya ukuu, si katika mantiki ya dini na ibada tu , lakini pia hata katika matendo ya dhati ya maisha yao ya kila siku.  Kwa maana hiyo katika masuala ya siasa hawali yote upo ulazima na dharura ya kuwa na mahusiano mema, ili kuhakikia kuwa unakuwepo ule usawa wa kijamii na heshima ya hadhi ya binadamu. Roho na mwili siyo vitu viwili kati yao vilivyotengena, bali ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba kwa  ishara ya hali ya juu katika uumbaji. Tendo la kukubali dhana hizi inatokana na kuheshimiana tamaduni na uwezo wa kuweka msingi wa pamoja ule  wa kuishi kwa amani.

Padre Checchin anathibitisha kuwa, kwa mujinu wa gazeti la National Giographic linaonesha kuwa; Bikira Maria ni mwanamke mwenye nguvu zaidi katika ulimwengu kwasababu ya ibada na mapokeo ya Mama Maria kukatisha karibu katika maendeo makubwa kijiografia. Hiy inajionesha katika  imani za dini, wakatoliki, waihindu na waislam. Na kwa njia hiyo dhana ya maisha imejikita katika thamani kubwa ya Maria na  kama makubaliano ya pamoja katika tamaduni hizo. Tassi ya Taalimungu ya Maria kwa dhati inayo wajibu na wito huo  wa kuelezeahali halisi, ili kutafuta na kutambua tamaduni, kuwa na akili ya kupokea, kukaribisha,kukutana, na kupenda tamaduni nyingine.

Akifafanua zaidi juu ya semina  ya  taalimungu ya Maria kwa wanadiplomasia wa Vatican anasema kuwa  inashinda zaidi ya thamani za semina nyingine za utambuzi: kwa maana inawakilisha hatua msingi za matendo wazi na dhati ya  Kanisa ili kusaidia utambuzi na maana  ya mazungumzo kwa ngazi ya dunia , katika kupinga vita ambavyo vimegewanyika katika maeneo mengi ya sayari hii. Hii ni shughuli nyeti ya kimataifa ambayo inajikita katika hali halisi ya sasa, wakati huo huo inajikita pia katika mpango mzima wa Papa Francisko anayetaka Kanisa kutoka nje.  Semina hii inathibitisha na kuonesha ushirikiano wa dhati kati ya Chuo Kikuu cha Antonianumu na Taasisi ya Taalimungu ya Maria kama umoja wa Kifransiskani na uwajibikaji katika kipindi hiki cha kihistoria.

Tarehe 24 Mei kutakuwa na maadhimisho ya kufunga semina mbili  yaani inayohusu,  Falsafa ya Amerika ya Kusini na  Taalimungu kwa wanadiplomasia wa Vatican. Kwa pamoja watahitimisha kwa Kongamano ambapo wanataweza pia kutoa zawadi kwa wanadipolasia, pia kuwasilisha mipango  yao ya pamoja ikiwa ni tunda la machakato wa safari ya mafunzo hayo.  Katika tendo la tukio hilo, litaudhuiwa na Kardinali Oscar Rodreguez Maradiaga, askofu Mkuu wa Hunduras, mmoja wa makardinali 9 washauri wa Baba Mtakatifu Francisko, pamoja na kutoa zawadi kwa wanadiplomasia pia atatoa tuzo la utambuzi wa Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu  ya Bikira Maria kimataifa.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.