2018-04-18 15:58:00

Mkutano mkuu wa Benki ya Dunia: Kipaumbele ni utu na maskini duniani


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya katekesi, Jumatano tarehe 18 Aprili 2018 ametoa wito wa aina mbili, kwanza kuhusu mkutano wa wahusika wa kifedha dunina kwa ajili ya maskini na wito wa pili  kwajili ya kufanya kila iwezekanavyo kutunza maisha  hasa wa  mtoto Alfie Evans na Vincent Lambert. Baba Mtakatifu akitoa wito juu ya mkutano wa Fedha Marekani, mara baada ya katekesi yake kuhusu Ubatizo amesema kwamba, Jumamosi utafanyika  mkutano wa Banki duniani huko Washington na  hivyo anawatia moyo katika juhudi za pamoja wahusika wa fedha ili watafute kuhamasha hali ya maisha hasa wale maskini na kuendeleza kwa dhati mendeleo kamili ya heshima ya hadhi ya binadamu!

Wito wa pili ulikuwa unatoa kuwa na  umakini wa maisha ya  Vincent Lambert na mdogo Alfie Evans. Na kuthibitisha kuwa, mkuu wa maisha tangu  kutungwa kwake hadi mwisho wa asili ni Mungu. Ni wajibu wetu kufanya kila iwezekanavyo  kutunza  maisha. Na kwa ukimya ameomba wote wasali ili maisha yaweze kuhshemiwa kwa kila mtu na zaidi kwa ndugu hao  wawili. Amewaalika watu wote ambapo kwa mujibu wa takwimu wanasema walikuwa ni waamini na mahujaji 17,000 katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko asubuhi na mapema ya tarehe 18 Aprili 2018 kabla ya kuanza Katekesi yake amekutana na  Thomas Evans, baba yake Alfie Evans, taarifa hizo zimeandikwa katika Gazeti la Nuova Bussola Quotidiana:http://www.lanuovabq.it/it

Katika Gazeti la Nuova Quotidiana linaandika kuwa, Tohamas Evan, Baba yake Alfie, amefika asubuhi na mapema mjini Roma, akisndizwa na mwandishi wa Gazeti hilo, Benedetta Frigerio, kukutana kwa faragha na Papa Francisko, na baadaye kuendelea na Katekesi katika uwanja  wa Mtakatifu Petro. Mkutano wa faragha umedumu kwa dakika 20. Makutano hayo kutokana na Askofu Francesco Cavina wa Jimbo la Carpi (MO) nchini Italia, ambapo pia  Papa Francisko amemkadhi  Askofu huyo, kuendelea na mahusiano kati ya Sekretarieti ya Vatican na wazazi wa mtoto huyo  kwenye mchakato wa kuhamisha mtoto  huyo katika Hospitali ya Bambin Gesu’ Roma. Katika mkutano na kijana huyo na Papa Francisko kwa lugha ya kingereza amemwambia kwamba,“pambana kwa ajili ya mtoto wako na kwa ujasiri kama  Mungu anavyo tetea watoto wake”.

Sr Angela Rwezaula 

Vatican News

 
All the contents on this site are copyrighted ©.