2018-04-18 15:32:00

Ishala ya Msalaba ni mhuri wa Kristo Mfufuka!


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Aprili 2018 ameendelea na katekesi yake kuhusu maisha ya Kikristo katika kipindi hiki cha Pasaka kwa kukazia Sakramenti ya Ubatizo. Kwa kufikiria ishala na maneno ya liturujia, tunaweze kuelewa neema na wajibu wa Sakrameti hiyo ya kwamba ni lazima kuigundua daima. Tunafanya kumbu kumbu hiyo wakati wa kunyunyizia maji ya baraka, ambapo inawezekana kufanya tendo hilo kila mwanzo wa Misa ya kila Domenika na kama ilivyo kawaida, wakati wa kurudia ahadi za ubatizo katika wa mkesha wa Pasaka. Kama inavyojitokezwa wakati wa maadhimisho ya ubatizo ni ule mwenendo wa kiroho kwa njia ya maisha yote ya wabatizwa; ni kuanzishwa mchakato mzima ambao unawezea kuuishi na muungano na Kristo katika Kanisa. Zaidi ni kurudi katika chemchemi ya maisa ya kikristo inayotusaidia kurudia  kugundua vema zawadi tuliyo ipokea siku ya Ubatizo wetu na kupyaisha wajibu wa kujibu kwa hali yoyote ile unayojikita nayo.

Kupyaisha wajibu, kutambua vema zawadi hiyo ambayo ni ubatizo, na kukumbuka siku ya ubatizo wetu. Jumatano iliyopita niliomba kufanya zoezi nyumbani kwa kila mmoja katika kukukumbuka siku ya ubatizo, ikiwa na maana ya tarehe ngapi nilibatizwa. Ninatambua kuwa baadhi yenu wanafahamu lakini wengine hapana, hivyo ni lazima kuuliza wazazi na watu wangine kama vile wasimamizi wa ubatizo, kueleza  siku ipi ya ubatizo huo. Hiyo ni kwasababu ya ni kama kuzaliwa upya katika ubatizo na kwa maana na hivyo ni kama sikukuu ya pili ya kuzaliwa na ni muhimu kuuliza tarehe ya ubatizo.

Ni utangulizi wa tafakari ya katekesi ya sehemu ya pili juu ya Ubatizo ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Aprili 2018 katika viwanja vya Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa  maelfu ya waamini na mahujaji kumsikiliza kutoka pande zote za dunia; ambapo sehemu ya pili ilikuwa inahusu “ishara za imani kikristo”. Kabla ya kuanza tafakari hili limesomwa Neno la Mungu:"Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho",(Yh 3,5-6).

Baba Mtakatifu akifafanua zaidi juu ya Ubatizo anasema kuwa, mwanzo wa ibada ya utangulizi, kwanza wanauliza jina la mwenye kubatizwa. Hii kwa kawaida ni ishara ya kukutana na mtu, unajitambulisha kwa jina haraka, ili kuondokana na kutotambulika. Bila jina unabaki bila kujulikana, bila kuwa na haki na wajibu. Mungu anamwita kila mmoja kwa jina lake, anapenda kila mmoja kwa nafsi yake na katika udhati wa historia yetu. Ubatizo unawasha wito binafsi wa kuishi kama mkristo, ambaye baadaye ataendeleza katika maisha yote. Ubatizo unawajibisha kutoa jibu binafsi, siyo kama kukopesha. Maisha ya kikristo kwa dhati yanajikita katika majukumu nyeti ya kuitwa na kutoa jibu. Mungu anaendelea kutamka jina letu, hata katika mchakato wa miaka kwa kutoa sauti ya  wito wake ili kuweza kufanana na Mwanae Yesu. Jina kwa hakika ni muhimu! Wazazi wanafikiria jina la kumpatia mtoto wao mapema kabla ya kuzaliwa; hata hiyo ni sehemu ya subiri ya mtoto ambaye kwa jina nafsi atakuwa na uzalendo asili hata ule wa maisha ya kikristo ambayo yamo ndani ya Mungu.

Kuwa mkristo ni zawadi inayotoka juu (taz Yh 3,3-8). Siyo rahisi kununua imani, badala yake ni ya kuomba na kupokea zawadi hiyo. “Bwana naomba zawadi ya imani, ni sala nzuri, Baba Mtakatifu amesisitiza , na ili kuwa na imani ni sala nzuri ya kuomba kila siku, ambayo huwezi kununua bali unaomba kwake. Ubatizo kwa hakika ni sakramenti ya imani ambayo waamini wanaangazwa na Roho Mtakatifu na kujibu kwa Injili ya Kristo. Ili kuweza kuikuza na kuamsha imani ya dhati katika jibu la Injili, ni lazima kuwafundisha wakatekumeni na kuwaandaa wazazi kama vile kusikiliza Neno la Mungu  wakati wa  maandhimisho hayo ya Ubatizo. Iwapo wakatekumeni ni watu wazima wao wako mstari wa mbele kuonesha  utashi wa kupokea zwadi ya Kanisa, lakini  kwa upande wa watoto wanawakilishwa na wazazi na wasimamizi wa ubatizo. Mahojiano  kati yao, yanasaidia na kuwakilisha utashi wa watoto wadogowanaopokea Ubatizo, pia kwa Kanisa kuwa na umakini wa kuadhimisha maadhimisho hayo. Kielelezo chote hicho ni ishala ya Msalaba, ambayo mwadhimishaji na wazazi  wanamwekea juu ya paji la uso wa mtoto. Ishala ya msalaba inaeleza muhuri wa Kristo juu ya wale ambao ni wake na kuonesha maana ya neema ya wokovu ambayo Kristo ameshinda  kwa njia ya msalaba wake.

Baba Mtakatifu Francisko katika ishara ya msalaba, amependelea kurudia suala hili kwamba mara nyingi watoto hawajuhi kufanya ishala ya msalaba na hivyo wazazi baba, mama, babu na bibi, wasimamizi wa watoto wa ubatizo lazima kuwafundisha watoto wafanye ishala ya msalaba  vizuri kwasababu wanarudia kile ambacho kilitendeka katika ubatizo: kwa kuwafundisha watoto wanafanya vizuri maana wanajifunza kutoka kwa watu wazima. Msalaba ni kielelezo cha kuonesha sisi ni kitu gani. Namna yetu ya kuongea, kufikiria, kutazama, kutenda yote ni chini ya ishala ya msalaba, kwa njia ya upendo wa Yesu hadi mwisho. Watoto wanatiwa ishara ya msalaba katika paji lao usoni. Wakatekumeni wazima, wanatia ishala hiyo hata ndani ya milango ya fahamu kwa maneno haya: Pokea ishala ya msalaba katika masikio ili kusikiliza sauti ya Bwana; kwenye macho ili kuona mwanga  wa uso wa Mungu; katika midomo , ili kujibu na kutangaza Neno la Mungu; katika kifua, kwasababu Kristo aweze kuishi kwa njia ya imani katika mioyo yenu; juu ya mabega, ili kuweza kuubeba mzigo mwepesi wa Kristo.

Unakuwa mkristo kwa kipimo cha Msalaba unavyojieleza ndani mwetu kama alama ya Pasaka (taz Uf 14,1; 22,4), ili kuweza kuonekana, nje na ndani ya mbele ya maisha ya mkristo. Kufanya ishala ya msalaba tunapo amka, kabla ya chakula , mbele ya hatari na mabaya, kufanya ishala ya msalaba kabla ya kulala kufanya ishala ya msalaba ni kudhihirisha kuwa na sisi na  wengine ni watu gani na tunataka kuwa wakina nani. Na ndiyo maana ni muhimu sana kuwafundisha watoto waweze kufanya vizuri ishala ya msalaba. Kama tufanyavyo ishala ya msalaba wakati tunaingia kanisani, ndivyo tunaweza kufanya hivyo hivyo hata tunapoingia ndani ya nyumba zetu, kwa kuendelea kuhifadhi hata maji yaliyobarikiwa. Na kila mara tunapoingia ndani ya nyumba au kutoka tunafanya ishala ya msalaba na maji hayo ikiwa na maana ya kutukumbusha kuwa sisi ni wabatizwa.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.