2018-04-17 15:12:00

Ujumbe wa Papa kwa Kongamano la 40 kitaifa la Caritas Jimbo Italia !


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican katika tukio la Kongamano la 40 la kitaifa kwa ajili ya  Caritas jimbo, ambalo  limefunguliwa tarehe 16-19 Aprili 2018. Baba Mtakatifu anasema, kongamano hilo, liweze kuwa daima chachu ya dhati kwa ajili ya wote hasa walio wa mwisho na masikini, hadi kufikia maeneo ya mwisho ya kuishi kwa binadamu na maisha ya kijamii ya sasa, hata wao waweze kuwa kweli mitume wa upendo.

Kadhalika katika ujumbe huo pia anawakumbuka wahanga wa Caritas italia hasa  Monsinyo Giovanni Nervo, mwenyekiti wa kwanza wa Caritas Italia, Monsinyo Giuseppe Pasini aliye fanya kazi kwa miaka 24 ndani ya Caritas Italia akiwa pamoja monsinyo  Nervo, karibu miaka 10  hivi na wengine mapadre wawili  wakereketwa, ambao katika mawazo na ushuhuda wa thamani ya maisha waliweza kutajirisha Kanisa la Italia kwa urithi ambao hadi sasa unazidi kutoa matunda ya dhati ya upendo na huruma.

Kongamano linafanyika huko Abano Terme, Padua nchini Italia ambapo wanashiriki zaidi ya wakurugenzi 600 na wahudumu 220 wa caritas majimbo, kwa kuongozwa na mada mwaka  2018: “ kijana ni… jumuiya mahali pa kushirikishana”.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.