2018-04-17 16:08:00

Tarehe 20 Aprili 2018 Papa Francisko atembelea Alessano na Molfetta Italia!


 “Ziara ya Baba Mtakatifu katika Kanisa la Ugento –Leuca na kutua katika kaburi la mtumishi wa Mungu Padre Tonino Bello ni zawadi inayotarajiwa na maalum. Ni mchango wa ushuhuda wa waamini na mfano wa kuigwa ambao alifanya katika Kanisa na zaidi kuwa karibu na watu”. Haya ni mameno ya Padre Beniamino Nuzzo Gombera za Seminari  ya Jimbo la Ugento, wakati akisimulia shauku na  maandalizi ya kuompokea Baba Mtakatifu Francisko katika ziara  yake   Ijumaa tarehe  20 Aprili 2018, ambapo atapata fursa ya kutembelea mji wa Alessano, mahali alipozaliwa mtumishi wa Mungu Askofu Tonino Bello, pia fursa ya kukaa kwa faragha katika kaburi lake na kukutana na waamini wa jimbo la Molfetta, mahali ambapo alitoa huduma kama mtumishi wa Mungu. Baba Mtakatifu atapapa kuadhimisha misa Takatifu na watu wa maeneo hayo.

Tukio la ziara yake katika maeneo haya ni katika kuadhimisha  miaka 25 tangu kifo cha Askofu Tonino Bello. Kiongozi wa Kanisa, aliyetambua kuhudumia watu kwa upendo mkubwa, kuanzia wadogo hadi wakubwa, na zaidi kwa maskini na wote ambapo wamo pembezoni mwa jamii. Watu wengi wanamkubuka kwa upendo huo na zaidi hata katika urithi wa roho yake, kupitia maandishi yake ambayo yanatia , moyo , yanatuliza  na kutoa chachu ya kuwa na matumaini katika Bwana.

 Alikuwa ni mwenye huruma kwa kila upande, alitambua mateso ya Kristo kwa njia ya mateso ya watu wake aliokutana nao siku na hivyo maandishi yake ni urithi mkubwa. Katika maandishi yake anasema,“kugundua na kujikita kwa upendo wa Mungu kwa  kina, kwa kila kiumbe, ina maana ya kupata maana ya maisha binafsi; si kwasababu ya kupata  faraja, bali  hata katika kuelekea kwenye furaha ya kweli na ndiyo maana sisi tumezaliwa”. 

Katika uzoefu wake wa kichungaji na changamoto za kila siku hasa katika ulimwengu wa mateso kuanzia katika naa na kiu ya maisha , Askofu Tonino Bello anaanduika: “kwa bahati mbaya katika ulimwengu wetu mahalia ambapo milioni 50 za watu wanakufa kila mwaka kwa njaa, mkate ni ishara ya muungano, wakati  huo huo mkate unageuka kuwa alama ya kutangazwa na pia kugeuka kuwa uhalifu mahali ambapo mantiki ya vita inapita”.
 
Kadhalika kwa kutazama umaskini, Askofu Tonino Bello anaandika: “ Kwa  umaskini, watu wanaamini tu wanapoona anayeishi kwa ajili ya wengine kwa maana ya tabia ya kushirikishana na kwamba “iwapo kisu kinaweza kukata shuka nusu na kumpatia mwingine,kama alivyofanya Mtakatifu Martino wa Tour, ni dalili za kuonesha hata ukuu wa kutoa kwa dhati nusu kipande cha vazi!

Kwa njia hiyo anasema kugundua watu watu maskini ni vigumu kwasababu wapo wengine ambao wanavaa sala kama ile ya shule.Na ili kuweza kutofautisha , wapo wale ambao wanavaa nguo maridadi zinazoshonwa kwa mitindo ya kisasa ili kuweza kuondokana na kufafanishwa. Na “ Kanisa ambalo halioti ndoto siyo Kanisa, bali ni kizingiti. Kwa maana haliwezi kutangaza habari njema na mpya kwa yule anayetafuta kwa matumaini wakati ujao. Ni kwa njia ya yule anayeota ndoto anaweza kuinjilisha ulimwengu huu.

Kwa maneno hayo mafupi, unaweza kutambua roho ya mtumishi wa Mungu Askofu Tonino Bello, vipo vitabu ni vingi vilivyo andikwa mawazo yake ya kila siku aliyokuwa akiandika baada ya tafakari. Kuanzia mwaka 1958 -1976 alikuwa ni msaidizi na Gombera wa Seminari ya Ugento. Miaka ambayo ni msingi katika maisha yake, ambapo aliweza kuongoza kwa majiundo na kiuchungaji bila kuchoka. Alikuwa ni mkristo wa kweli, padre na askofu maalum, kwasababu alikuwa na upendo wa Kristo, wa Kanisa na wa kibinadamu, zaidi walio maskini na kubaguliwa. Alikuwaakitoa sauti kwa niaba ya wale wasio kuwa na  sauti, hadhi na haki, kwa namna  hiyo hata kama wale ambao ni kama jiwe lililowekwa pembeni. Alifundisha kukimbilia katika imani ambayo pamoja na changamoto zake.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.