2018-04-17 15:43:00

Matashi na baraka kwa Papa Mstaafu Benedikto XVI kufikisha miaka 91!


Tarehe 16 Aprili 2018 ilikuwa ni siku maalum ya kukumbuka miaka 91 ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliyezaliwa  mnamo tarehe 16 Aprili 1927 huko Maektl nchini Ujerman. Akachaguliwa kuwa katika kiti cha kharifa wa mtume Petro mnamo tarehe 19 Aprili 2005. Na tarehe 11 Februari 2013 alitangaza uamuzi wake wa kustaafu, ambamo mnamo tarehe 28 Februari 2013  akawa Papa mstaafu.

Wakati wa kusheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa ameungana na kaka yake Monsinyo George katika hali ya utulivu na kifamilia. Kwa heshima yake, walipiga bendi ya musiki, kikosi cha ulinzi  wa Uswis  wa Vatican ambapo wametumbuiza baadhi ya nyimbo mbali mbali katika makao anapoishi Monasteri ya Mater Ecclesiae Vatican. 

Na wakati wa Misa ya asubuhi ya tarehe 16 Aprili 2018, Baba Mtakatifu Francisko ametolea kwa ajili ya Papa Mstaaafu Benedikto XVI na baadaye kumtumia salam za matashi mema.

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News!

 
All the contents on this site are copyrighted ©.