2018-04-16 16:00:00

Ziara ya Papa Francisko katika Parokia ya Mt.Paulo wa Msalaba,Roma!


“Mitume walikuwa wanatambua kuwa Yesu kafufuka, kwasababu Maria Magdalena alikuwa amewataarifu asubuhi na mapema, Petro alikuwa ameona na hata mitume wawili walikuwa wamerudi kutoka Emau, ambao  walikuwa wamesimulia juu ya  kukutana na Yesu Mfufuka. Walikuwa wanatambua kuwa amefufuka na yuko hai. Pamoja na hayo ukweli huo ulikuwa bado haujaingia ndani ya mioyo yao. Japokuwa walikuwa wanatambua ukweli, lakini walikuwa na wasiwasi. Labda walipendelea kubaki na ukweli katika akili yao. Ni hatari ndogo kubaki na ukweli akilini, badala ya kuwa nao katika moyo….. Na mitume wote walikuwa wameunganika kwa pamoja na ndipo akatokea Bwana. Mwanzo waliogopa sana wakidhani ya kwamba wanaonaroh, lakini Yesu mwenyewe akawambia: “mbona mnafadhaika tazameni, nishikenishikeni, mwone kovu zangu, kwa kuwa roho haina mwili na mfupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo”, ( Lk 24,35-48).

Ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 15 Aprili 2018 wakati wa Ibada ya Misa Takatifu, alipotembelea Parokia ya Mtakatifu Paulo wa Msalaba huko Corvial  Roma, ikiwa ni mojawapo ya ziara zake  nyingi za kitume anazozifanya kila wakati kutembelea Jimbo mahalia la Roma.  Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na mahubiri ya siku kutoka katika Injili ya Mtakatifu Luka anasema:  Yesu aliwatokea mitume wake baada ya kufufuka, lakini je ni kwanini walikuwa na wasiwasi?  Injili inatoa maelezo kamili, kwamba, basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaaajabu”,  hii ni kutokana na furaha hadi kuwashangaza kiasi cha kutokuweza kuamini , maana ilikuwa ni furaha kubwa mno! 

Baba Mtakatifu anasema, furaha hiyo inaweza kufanana hata na sisi, iwapo tunaweza kupokea habari  fulani mpya. Kabla ya kuipokea ndani ya roho, tunajiuliza hivi ni kweli,na kujiuliza maswali mengi aliyekutapia habari hiyo, je umetambuaje? Je umesikia wapi?  Kuufanya hivyo ni kutaka kuhakikisha kwamba kile unachoelezwa ni ukweli, ni furaha kubwa! Hayo yanatokea kwa wote na hata kwa kile kilicho kodogo sana, lakini fikirieni furaha ya mitume hao! Baba Mtakatifu anaongeza… Ilikuwa ni furaha kubwa sana ambayo hadi kufikia kwamba si rahisi kuamini machoni. Pamoja na hayo wao walikuwa na bahati kubwa kwasababu Bwana alikuwa pale pale. Na tukio hilo lisingewaacha na utofauti  yaani ukweli kuingia ndani ya mioyo yao kwa kile ambacho walikuwa sasa wanatazama, na ndiyo maana hatimaye waliamini. Baba Mtakatifu ansisitiza; huo ndiyo upyaisho wa ujana ambao Bwana anatujalia!

Katika maombi ya utangulizi wa misa imesikia, sala juu ya upyaisho. Sisi tumezoea, kuzeeshwa na dhambi, kwa maana dhambi inazeesha moyo daima. Inatufanya moyo uwe mgumu, uzeeke  na kuchoka. Dhambi inachosha moyo na kupoteza kidogo imani ya Kristo mfafuka. Na ndiyo maana katika somo la pili, Mtakatifu Yohane anasema na “kama mtu akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki”. Kwa maana hiyo hakuna hofu kwa maana ni kumwendea Yeye anayesamehe dhambi na kupyaisha. Dhambi inazeesha lakini tunapokaribia Yesu mfufuka na aliye hai, anapayaisha maisha yetu. Ndiyo nguvu ya Yesu mfufuka, hasa tunapokaribia sakramenti ya kitubio,  ni kwajili ya kupyaisha na kuwa vijana. Yesu mfufuka anafanya hivyo, Yeye yupo katikati ya wote , katika altare na katika Neno lake. Ni vema kushangilia wote kwamba amefufuka, yeye anataka kuwa mtetezi, maana ni mwakili tunapokuwa na dhambi ili kuweza kupyaisha maisha yetu.

Baba Mtakatufu amesisitiza kuomba neema kwake Kristo aliye hai kwa maana amefufuka!. Ndiyo maana yake na iwapo tunaamini hilo, mambo mengine ni ziada. Yeye ndiye maisha yetu na ujana wetu. Ni muhimu kumwamini Yesu aliye hai  unapopokea Ekaristi na kuwa na utambuzi ya kwamba Kristo ni mshindi wa dhambai na yupo kati yetu, na iwapo utakuwa na imani hiyo basi ndiyo kusema wewe ni mkristo mwema.

Baba Mtakatifu amehitimisha akiomba waamini wote kuwaomba neema ya kuguswa na Yesu mfufuka, kukutana naye wakati wa sala, wakati wa sakramenti, wakati wa kitubio ambacho kinapyaisha  ujana wa Kanisa, kwa njia ya kuwatembelea wagonjwa, wafungwa na wale wenye kuhitaji zaidi, watoto na wazee. Iwapo unahisi kufanya jambo lililo jema ni Yesu mfufuka anayetoa chachu na msukumo wa kufanya hivyo. Ndiyo neema ya kuomba katika jumuiya yenye furaha na kila mmoja ili aweze  kukutana naye kwa imani.

Sr Angela Rwezaula
 Vatican News!

 
All the contents on this site are copyrighted ©.