2018-04-12 15:52:00

Unicef nchini Israeli inaomba ulinzi wa watoto katika Ukanda wa Gaza!


Siku kumi za mwisho watoto watatu wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa. Robo moja ya watoto (250.000) wanahitaji msaada wakisaikolojia  huko Gaza na  nusu ya watoto wengi wanahitaji msaada wa watu wakubwa.

Huu ni uthibitisho kwa mujibu wa Geert Cappelaere, Mkurugenzi wa Kanda ya UNICEF  wa Nchi za Mashariki na Afrika Kaskazini. Akielezea hali halisi ya ghasia zinazoikumba nchi hiyo kwamba, kwa siku nyingi watoto huko Gaza wanaishi hali mbaya sana. Ni lazima wadau wote kila sehemu kuweka kipaumbele cha kulinda watoto. Watoto wasiwe kama chanzo cha ghasia hata kuwekwa hatarini au kuwalazimishwa washiriki katika vurugu.

Katika siku hizi za mwisho hali mbaya na ngumu inazidi kuongezeka huko Gaza mahali ambapo Familia nyingi wanaish bila umeme. Kati ya vijana ambao wanaishi karibu kwa miaka 10  na mizunguko mitatu ya migogoro ya vita, ukosefu wa ajira umekuwa mkubwa kwa asilimia 60%, na aslimia 10% ya familia huko  Gaza hawana maji salama ya kunywa. Wakati watoto wengi wanahitaji msaad wa kisaikolojia  kutokana na mateso waliyopata ya vita, maana watoto hao pia wanategemea mahitaji yao ili waweze kuisha hata kwa siku.

Pamoja na hayo Unicef kwa sasa imeweza  kuwapatia vifaa muhimu vya afya huko Gaza, vilivyokuwa vinategemewa kwa muda mrefu. Pia Unicef inajitahidi kuwasaidia wazazi juu ya uwezekano wa kuweza kuwasaidia kisaikolojia vilevile katika huduma ya afya, maji , elimu na ulinzi japokuwa bado ipo haja na dharuara ya watu hawa, kwa mujibu wa Unicef.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News!
All the contents on this site are copyrighted ©.